Simba wapewa nondo kuiua Nkana

NA ZAINAB IDDY

BAADA ya kufanya vizuri katika mechi za hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepewa siri za kuwakabili wapinzani wao wajao, Nkana FC ya Zambia katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Simba SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1, ikishinda mabao 4-1 jijini Dar es Salaam na mabao 4-0 ugenini Jumanne ya wiki hii.

Mechi ya kwanza dhidi ya Nkana itafanyika mjini Kitwe kati ya Desemba 14 na 16, wakati marudiano yatakuwa kati ya Desemba 21 na 23 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

 Wakizungumza na BINGWA kwa nyakati tofauti, wachezaji wa zamani na wachambuzi wa soka nchini, wamesema kuwa Simba hawapaswi kuingia kichwa kichwa katika mchezo wao dhidi ya Nkana FC.

Ally Mayay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa soka nchini, alisema: “Simba na Nkana zilishawahi kukutana miaka iliyopita. Ifahamike kuwa Nkana ilishafika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1990, lakini pia ina wachezaji wengi kutoka nchi zilizoendelea kisoka tofauti na Simba.

“Ili Simba waweze kushinda mbele ya Nkana, ni lazima wajipange upya kwa kurekebisha makosa ambayo yalijitokeza hususan kwenye safu ya ulinzi ambayo licha ya kutofungwa kwenye mechi za kwanza, lakini inahitaji maboresho kwani wangekutana na timu nzuri wasingefika walipo sasa,” alisema.

Naye kocha Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’, alisema: “Simba bado ina kazi kubwa na kila wanavyosonga mbele lazima wajue ndio ugumu wa mashindano unavyoongezeka, hivyo benchi la ufundi linatakiwa kukaa na wachezaji ili kuwaeleza nini kilichopo mbele yao.

“Ni vema Simba wakaenda kucheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa kwani Nkana ni timu nzuri kuliko hata Mbabane, wana uzoefu na mashindano na wamekuwa wakifanya vema katika mechi nyingi za kimataifa.”

Hiiitakuwa mara ya tatu kwa timu hizo kukutana katika michuano hiyo na katika marambili zilizopita, Simba ilitolewa na wakali hao wa Zambia.

Maraya kwanza ilikuwa mwaka 1994 katika robo fainali na mara ya pili, ilikuwa mwaka2002 raundi ya kwanza ya michuano hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*