googleAds

SIMBA SC JIANDAENI KISAIKOLOJIA

NA SAADA SALIM


 

KITENDO cha uongozi wa Simba kusitisha mkataba wa kocha msaidizi wao, Masoud Djuma, kimemwibua straika wa Stand United, Alex Kitenge, akisema Mrundi huyo atatua Yanga hivyo Wekundu wa Msimbazi hao hawana budi kujiandaa kisaikolojia.

Akizungumza na BINGWA jana, Kitenge alisema anamfahamu Djuma kwani kocha huyo amewahi kumfundisha katika kikosi cha vijana cha Rwanda, hivyo kutokana na uwezo wake akitua Yanga ataibadilisha mno timu hiyo na kuifanya kuwa tishio.

“Kitendo cha Simba kumwachia Djuma wanatakiwa kujipanga kama atachukuliwa na Yanga au kwenda katika timu nyingine hapa hapa nchini, kwani atapania kufanya mambo makubwa ili kuwasuta viongozi wa Simba.

“Nafahamu juu ya uwezo wake wa kufundisha, pia amekuwa kocha wa mafanikio pale anapopewa uhuru katika timu kama ilivyokuwa Rayon Sports ya Rwanda na Simba msimu uliopita alipoiwezesha kuchukua ubingwa wa ligi,” alisema.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.
Previous Article

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*