SILVA: ARSENAL NAO WAMO MBIO ZA UBINGWA

MANCHESTER, England


 

KIUNGO wa timu ya Manchester City, Bernado Silva, amezitaja timu nne zenye uwezo wa kuipa upinzani klabu yake kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, ikiwemo timu ya Arsenal.

Silva na City yake wana jukumu zito la kutetea ubingwa wao msimu huu, baada ya kuweka rekodi ya kipekee msimu uliopita waliponyakua taji la ligi hiyo kwa kukusanya pointi 100.

Hadi sasa vijana hao wa kocha, Pep Guardiola, wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 26, wakilingana na Liverpool, huku wakifuatiwa na Chelsea (pointi 24) na Arsenal (22).

Spurs wao wanakamata nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.

“Kwanza itambulike kwamba msimu huu ni mgumu sana kwetu kushinda tena Ligi Kuu,” alisema Silva.

“Lakini tutajituma kila mechi tuweze kushinda ingawa Chelsea na Liverpool nazo zipo kwenye vita hii, Arsenal na Tottenham pia siwezi kuzisahau,” aliongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*