googleAds

SHONZA AMVULIA KOFIA WEMA

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema filamu ya Day After Death (D.A.D) ya Wema Sepetu na Van Vicker kutoka Ghana, imekuja na vitu tofauti ambavyo vinapaswa kuigwa.

Shonza aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipohudhuria sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Wema, iliyoambatana na uzinduzi wa filamu uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na kupambwa na mastaa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Shonza alisema: “Alipotoa filamu yake ya Heaven Sent mwaka jana niliiona na kuikubali ndiyo maana nikasema nije niitazame Day After Death, kwa sababu naamini itakuwa nzuri na ubora wa hali ya juu pia Wema atakuwa amejifunza vitu vingi kutoka kwa Van Vicker,” alisema Shonza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*