SHONZA AKABIDHI ZAWADI WASHINDI CLUB RAHA LEO

NA CRISTOPHER MSEKENA


 

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amekabidhi zawadi kwa washindi sita walioibuka kidedea kwenye shindano la kusaka vipaji la Club Raha Leo msimu wa nne, lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa Kibo Complex, Tegeta, Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi za hundi ya shilingi 5,000,000  na cheti cha sanaa, Shonza aliyekuwa mgeni rasmi aliwataka wadau wa muziki, wasanii wakubwa na bendi hapa Tanzania kuvitumia vipaji hivyo.

“Niombe mashirika na makampuni na vyombo vya habari kuanzisha mashindano kama hayo, lakini pia niwapongeze majaji Innocent Nganyagwa (Ras Inno), Mariam Migomba, Beatus Nsiima, Nyoshi El Sadat na wote kwa kutenda haki,” alisema Julianza Shonza.

Washindi hao ni William Mseti (Afro Pop), Mwatano Ally (Taarabu), Arnod (Ngoma Zetu), Oliver Mushi (Rhumba), Suleiman Abdallah (Bongo Fleva) na Omari (Bongo Fleva).

Fainali hizo zilihudhuriwa na mastaa wengi wa Bongo Fleva akiwamo Barnaba, Shetta na Beka Flavour.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*