googleAds

SHIMMUTA kuwapiga msasa wadau, viongozi

Victoria  Godfrey

SHIRIKISHO la Michezo la Mashiriki ya Umma , Taasisi na Kampuni  Binafsi (SHIMMUTA), lina mpango wa kuendesha semina kwa viongozi  na wadau itakayofanyika kati ya Agosti na Septemba mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Naibu Katibu Mkuu wa SHIMMUTA, Twaib  Dowile, alisema itasaidia  viongozi  kufahamu majukumu na  kutekeleza wajibu wa  taaluma zao.

Dowile alisema  semina hiyo, itawajengea uwezo katika kukabiliana na changamoto  ya  mtazamo hasi kipindi cha michuano.

Alisema  changamoto kubwa kwa baadhi ya wadau na viongozi hawafahamu  kutafsiri sheria na kanuni za michezo  hivyo wakipatiwa semina hiyo itasaidia kupunguza malalamiko mbalimbali katika michuano inayoandaliwa na shirikisho hilo.

Dowile alisema semina hiyo itakuwa ni sehemu ya  maandalizi ya michuano ya SHIMMUTA itakayofanyika mwaka huu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*