googleAds

Shime aahidi kuendeleza ubabe Tunisia

NA TIMA SIKILO

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Tanzania, ‘Twiga Stars, Bakari Shime, ameahidi kuendelea kufanya vyema katika  michuano ya Kanda ya Kaskazini  (UNAF) inayoendelea nchini Tunisia.

Mpaka sasa Tanzania imeshacheza michezo miwili na kufanikiwa kupata ushindi katika michezo yote hiyo.

Mchezo wao unaofuata unachezwa leo katika dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Kram nchini humo.

Akizungumza na BINGWA jana Shime alisema wanakutana na changamoto nyingi katika michezo yao lakini wanakabiliana nazo nakuhakikisha kuwa wanaendelea kufanya vizuri.

Alisema kuna muda wanakutana na watu ambao wamewazidi baadhi ya vitu lakini wakishawasoma kipindi cha kwanza  na baadaye mambo yanakuwa yanaenda vizuri.

“Kuna timu ambazo tunakutana nazo zina changamoto lakini sisi tunazisoma na kujua nini tufanye ili kuwamudu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*