Shearer aivulia kofia Arsenal

LONDON, England

ALAN Shearer ameisifia Arsenal baada ya kuichapa Hull City kwenye mchezo wa Jumamosi ya wiki iliyopita.

Gunners walishinda mabao 4-1 kwenye Uwanja wa KC dhidi ya kikosi ambacho mchezaji wao, Jake Livermore alitolewa kwa kadi nyekundu.

Lakini Shearer alisema kadi nyekundu imeleta mabadiliko madogo kwenye matokeo.

Akiwa kama mchambuzi wa mechi hiyo kwenye moja ya vituo vya televisheni nchini England, alisema: “Arsenal walikuwa vizuri. Wangeweza kushinda hii mechi hata kama wangekuwa 11 kwa  11.

“Wameweka watu wengi pale mbele. Pasi zao zilikuwa na malengo, walicheza ‘one touch’ au ‘two touch’ wakitafuta nafasi.

“Wangeweza kulegeza baada ya Hull kubaki wachezaji 10, lakini waliendelea kucheza kwa kiwango cha juu. Arsenal walikuwa watamu sana.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*