SHARAPOVA ATINGA RAUNDI YA TATU US OPEN

WASHINGTON, Marekani

STAA wa tenisi, Maria Sharapova, ametinga raundi ya tatu ya michuano ya US Open kwa kumfunga Timea Babos.

Katika mchezo huo, Sharapova aliibuka kidedea kwa ushindi wa seti 6-7 (4-7) 6-4 6-1.

Sharapova, aliyekuwa na skendo ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni, alilazimika kutumia nguvu ya ziada kumshinda Babos, ambaye alionekana kujipanga.

Baada ya ushindi huo, mwanadada Sharapova anatarajiwa kukutana na Sofia Kenin au Sachia Vickery katika hatua ya mtoano.

“Ni siku nzuri kwangu, nimepambana kwa nguvu zote ili niweze kushinda. Nashukuru nimefanikiwa na kuendelea hatua inayofuata,” alisema Sharapova


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*