Serikali yatoa ushauri kwa klabu, wachezaji

NA ZAINAB IDDY

SERIKALI kupitia Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo, imewataka viongozi wa klabu kukaa na wachezaji kwa lengo la kuangalia namna ya kulinda mikataba yao.

Akizungumza na BINGWA juzi, Singo alisema itakuwa ni vizuri kama hilo litafanyika kwa sababu haijulikani janga la Corona litaisha lini na baadhi ya wachezaji mikataba yao imekaribia kumalizika.

Singo alisema  hawajui baada ya serikali kutangaza kusisitisha shughuli za michezo kwa siku 30  hajui lini hali itakuwa nzuri au la.

“Mfano katika mpira wa miguu timu zimeingia mikataba na wachezaji na huenda msimu huu ilikuwa ifike mwisho lakini kwa sababu ligi zimesimama na haijulikani itaendelea lini si vibaya wakakaa mezani na kuzungumza.

“Nasema hivi kwa sababu tutakuja kusikia kesi za wachezaji kugoma kucheza kwa sababu mikataba imekwisha wakati hakukuwa na kazi inayofanyika,” alisema Singo

Singo alisema katika hilo busara ya pande mbili  kwa maana ya wachezaji na waajiri wao  inahitajika ili baadaye kusiwapo mgogoro wa kimaslahi.

“Hii haitakiwi kufanyika katika soka pekee, ni katika michezo yote ambayo viongozi wameingia mikataba na watendaji kazi wao,”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*