googleAds

SERENGETI BOYS WAIBANA MALI

Libreville, Gabon

TIMU ya Tanzania ‘Serengeti Boys’, imewabana mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, Mali na kutoka nao sare ya 0-0, katika mchezo wa Kundi B uliopigwa jana Uwanja wa I’Amitie Sino-Gabonaise, mjini Libreville, nchini Gabon.

Matokeo hayo yalikuwa muhimu sana kwa Serengeti Boys, ambao ndio walikuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya vijana barani Afrika.

Hakukuwa na hatari yoyote langoni mwa Junior Eagles wala Serengeti Boys, lakini Mali, walitawala kipindi cha kwanza chote cha mchezo huo, huku safu ya ulinzi ya Serengeti Boys iliyokuwa ikiongozwa na Dickson Nickson Job, ikifanikiwa kumaliza kwenda mapumziko bila ya kuruhusu bao.

Serengeti Boys walirejea kipindi cha pili kwa kasi na kuonyesha umakini kwenye eneo la ushambuliaji, lakini baadaye Junior Eagles walipata nguvu na kuanza kutawala tena mchezo, wakati Mohamed Camara na Lassana N’Diaye wakipoteza nafasi za mabao kwa Mali na mechi hiyo ya kwanza ya Kundi B kumalizika kwa sare ya 0-0.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*