SERENGETI BOYS KUSHIRIKI COSAFA

    NA WINFRIDA MTOI


 

TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imealikwa kushiriki  michuano ya soka ya nchi za kusini mwa Afrika (Cosafa), yanayotarajiwa kuanza Desemba 7-29, mwaka huu, nchini Botswana.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha wa kikosi hicho, Oscar Milambo, alisema kutokana na mwaliko huo, wanatarajia kuingia kambini Septemba 22, mwaka huu.

Milambo alisema wamefurahi kupata mwaliko huo kwa sababu itawapa nafasi ya kucheza na timu za ukanda mwingine, tofauti na zile walizozoea za Afrika Mashariki.

“Tuliwahi kupata mwaliko wa kwenda Algeria katika mashindano ya vijana, lakini yaliahirishwa tukashindwa kwenda, hivyo hii ya Cosafa tunatarajia kuitumia vizuri kwa maandalizi ya Afcon 2019,” alisema Oscar.

Alisema wamekuwa na changamoto  mbalimbali, lakini kufanya vizuri kwa vijana wake imekuwa chachu ya kupata mialiko ya nchi tofauti.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*