googleAds

Scholes alimwa faini

LONDON, England 

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, ameambiwa na Chama cha Soka cha England (FA), kulipa faini ya kitita cha pauni milioni 8 (sh bil.22).

Scholes alikumbwa na hatia hiyo baada ya kujiingiza katika masuala ya kubeti na kukiuka sheria ya mchezo huo mwaka 2015.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Scholes aliomba radhi na kukubali kutoa kiasi hicho cha fedha.

“Naomba radhi kwa yote yaliyojitokeza, nafahamu nimetenda kosa na sitopinga kuhusu hilo,” alisema Scholes.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*