googleAds

SARE YA TATU YAMCHANGANYA GATTUSO

MILAN, Italia


 

JUZI AC Milan waligawana pointi na Empoli, ikiwa ni sare ya tatu mfululizo kwa kikosi hicho tangu kuanza kwa msimu huu wa Serie A.

Mwenendo huo umemchefua kocha wake, Gennaro Gattuso, ambaye sasa amewataka vijana wake kuamka.

“Kwa sasa hatuwezi kujiita timu kubwa. Timu kubwa inajitambua na ni ngumu (kufungika),” alisema Gattuso katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Sky Sport.

Hata hivyo, kocha huyo alikataa kumtupia lawama beki wake, Alessio Romagnoli, ambaye wakati AC Milan wakiwa mbele kwa bao 1-0, kosa lake liliiwezesha Empoli kusawazisha.

“Makosa yanaweza kutokea, lakini tunatakiwa kuamka na kuachana nayo haraka iwezekanavyo,” aliongeza.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*