RONALDO, SERGIO, HAZARD WAPETA TUZO BALLON D’OR

PARIS, Ufaransa


 

MASTRAIKA wa timu za Juventus na Manchester United, Cristiano Ronaldo na Sergio Aguero, ni miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kushindania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.

Majina ya wachezaji hao yalitangazwa jana na waandaaji wa tuzo hizo na huku wakiwataja nyota wa  Chelsea, Eden Hazard na N’Golo Kante, staa wa Real Madrid, Gareth Bale pia kuwania tuzo hiyo.

Ballon d’Or ni tuzo mashuhuri ambayo imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1956 na hutolewa kwa mchezaji bora zaidi wa mwaka wa kiume duniani.

Sherehe ya kumtangaza mshindi itafanyika mjini Paris Desemba 3, mwaka huu na mchezaji bora wa kike duniani pia atatunukiwa kwa mara ya kwanza.

Wachezaji wengine waliotajwa kuwania tuzo hiyo na timu zao kwenye mabano ni Alisson (Liverpool), Karim Benzema (Real Madrid), Edinson Cavani (PSG), Thibaut Courtois (Real Madrid) na  Kevin de Bruyne (Manchester City).

Mastaa wengine ni Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Isco (Real Madrid), Harry Kane (Tottenham), Roberto Firmino (Liverpool) na   Diego Godin anayekipiga Atletico Madrid.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*