googleAds

Ronaldo achafukwa kisa shabiki

TURIN, Italia 

NYOTA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amechukizwa na shabiki aliyeingia uwanjani, kwa ajili ya kutaka kupiga naye picha usiku wa kuamkia jana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen.

Baada ya shabiki huyo kuingia uwanjani, polisi walimvamia kwa lengo la kumtoa, lakini katika purukushani hizo, shabiki huyo alimkwaruza Ronaldo shingoni jambo ambalo hakupendezwa nalo.

Katika mchezo huo, Juventus walishinda 2-0 mabao yakifungwa na Cristiano Ronaldo na Gonzalo Higuain huku mpishi wa mabao hayo akiwa Paulo Dybala.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*