RONALDINHO KUOA WAKE WAWILI

RIO, Brazil


 

MKONGWE wa soka, Ronaldinho Gaucho, anatarajia kufunga ndoa na wanawake wawili kwa mujibu wa ripoti zilizopo nchini Brazil.

Mkali huyo wa zamani wa Milan na Barcelona, aliripotiwa kuwa yupo kwenye mipango ya kuvalishana pete za ndoa na ‘wachumba’ wake wawili, Priscilla Coelho na Beatriz Souza.

Warembo hao wamekuwa wakiishi na Ronaldinho ‘kwa furaha mno’ tangu Desemba mwaka jana katika jumba lake la kifahari lenye thamani ya pauni milioni tano, lililopo Rio de Janeiro.

Ronaldinho alianza kutoka na Beatriz mwaka 2016, lakini aliendelea kuwa na Priscilla ambaye alimpata miaka kadhaa iliyopita na kwa mujibu wa ripoti, wawili hao ‘wanalipwa’ takribani pauni 1,500 za kutumia watakavyo.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*