RODRIGUEZ AMKINGIA KIFUA ULREICH

MUNICH, Ujerumani    |   

STAA James Rodriguez amemkingia kifua mwenzake, Sven Ulreich, akisema kuwa, hapaswi kulaumiwa kwa kosa alilofanya la kuwazawadia bao Real Madrid na kuwafanya watupwe nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Juzi Bayern iliweza kulazimisha sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini dhidi ya Real Madrid, lakini wakajikuta wakitolewa kwa jumla ya mabao 4-3.

Katika mchezo huo, Ulreich alimzawadia Karim Benzema bao ambalo lilisababisha kufutwa la mapema ambalo lilifungwa na Joshua Kimmich na pia akashindwa kuzuia mpira wa pasi aliotengewa na Corentin Tolisso dakika ya 21 ya kipindi cha pili cha mchezo huo, ambao ulipigwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

James, ambaye yupo kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Real Madrid, aliweza kusawazisha tena, lakini matokeo hayo hayakuwafanya wasonge mbele.

“Huwezi kumlaumu golikipia kwa sababu alishatuokoa mara nyingi . Tulishafanya makosa katika mchezo wa kwanza ,” James aliliambia Shirika la Habari Hispania, AS.

“Nadhani leo tulikuwa na nafasi nzuri ya kushinda. Lakini kama Real Madrid wamefanikiwa kusonga mbele watakuwa wamefanya vizuri kuliko sisi,” aliongeza nyota huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*