googleAds

RIYAMA AFURAHIA KUNOGESHA ‘KAOLEWA’ YA ROSTAM

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII mahiri wa filamu nchini, Riyama Ally, amesema anafurahi kuona mashabiki wa muziki wamempokea vyema baada ya kuweka vionjo katika wimbo, Kaolewa, kutoka kwa wasanii Roma Mkatoliki na Stamina wanaounda umoja ujulikanao kama Rostam.

Akizungumza na Papaso la Burudani hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Riyama alisema alipata nafasi ya kuweka kionjo katika wimbo huo unaofanya vizuri kwa sasa baada ya uongozi wa Rostam kuona anaweza kuigiza na kuongea maneno ya uswahilini.

“Meneja wa Rostam alinipigia akaniambia kuna sauti inatakiwa niingize kwenye wimbo wao, nikafika studio nikaingiza kile kionjo chini ya usimamizi wa mume wangu na nashukuru wimbo ulipotoka umependwa,” alisema Riyama.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*