Rio azidi kumuunga mkono Solskjaer

MANCHESTER, England

BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini utakuwa ujinga endapo bodi ya klabu hiyo, itamtimua kazi kocha anayekinoa kikosi hicho Ole Gunnar Solskjaer.

Tangu msimu umeanza Man United imekusanya jumla ya pointi tisa, wakiwa wamecheza mechi nane za Ligi Kuu England.

Imeripotiwa takwimu hizo ni mbovu, kuwahi kutokea tangu miaka 30 iliopita Old Trafford, hata hivyo beki huyo wa zamani wa timu ya taifa England, ameendelea kumtetea na kumuunga mkono Solskjaer.

“Kila mtu anafahamu mambo yalivyo, utakuwa msimu mgumu, kumfukuza Solskjaer sio njia sahihi, nitashangaa nikiamka asubuhi na kusikia amefukuzwa kazi, hili jambo ni la muda mrefu, muhimu kuwa wavumilivu,” alisema Rio.

Man United itarudi baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa ambapo itashuka dimbani kumenyana na Liverpool, Oktoba 20 mwaka huu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*