Rio azidi kumuunga mkono Solskjaer

MANCHESTER, England

BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, anaamini utakuwa ujinga endapo bodi ya klabu hiyo itamtimua kocha anayekinoa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer.

Tangu msimu umeanza, Man United imekusanya pointi tisa wakishuka uwanjani kucheza mechi nane za Ligi Kuu England.

Imeripotiwa takwimu hizo ni mbovu kuwahi kutokea kwa miaka 30 Old Trafford, hata hivyo beki huyo wa zamani wa timu ya taifa England, ameendelea kumtetea na kumuunga mkono Solskjaer.

“Kila mtu anafahamu mambo yalivyo, utakuwa msimu mgumu, kumfukuza Solskjaer sio njia sahihi, nitashangaa nikiamka asubuhi na kusikia amefukuzwa kazi, hili jambo ni la muda mrefu, muhimu kuwa wavumilivu,” alisema Rio.
Mechi ya kwanza ya Man United baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa ni Oktoba 20 mwaka huu dhidi ya Liverpool.
@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*