Real Madrid waeleza kinachomsumbua Isco

MADRID, Hispania

TIMU ya Real Madrid imesema kwamba nyota wao Isco anasumbuliwa na matatizo ya shingo na mgongo na ndio maana hakuwamo katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid.

 Nyota huyo hakuwamo kwenye kikosi cha Santiago Solari ambacho Jumamosi  kiliivaa Atletico Madrid na mabao yaliyofungwa na nyota wao, Casemiro, Sergio Ramos na Gareth Bale yakawapa ushindi wa mabao 3-1.

Isco amekuwa akishindwa kupata nafasi ya kucheza tangu Solari alipochukua mikoba ya Julen Lopetegui na huku kocha huyo wa Real Madrid akionekana kumponda kwa kushindwa kujituma mazoezini na ndio maana amekuwa hampi nafasi ya kutosha.

“Katika soka unapaswa kujituma na kuelekeza kipaji chako kwa kila kitu,” Solari alisema kabla ya mchezo huo wa  El Derbi. “Unapaswa kufanya hivyo mazoezini na hivyo utapata nafasi ya kucheza,” aliongeza kocha huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*