Rayvanny agawa mafuta kwa bodaboda

NA BRIGHER MASAKI

MKALI wa Bongo Fleva, Raymaond Mwakyusa ‘Rayvanny’, ameendelea kujiweka karibu na mashabiki zake mara baada ya jana kugawa mafuta kwa madereva bodaboda na bajaji katika sheli ya State Oil, iliyopo Sinza Afrikasana, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mashabiki zake katika tukio hilo lililowavuta watu wengi, Rayvanny alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaamini waendesha bodaboda ni mashabiki zake wakubwa na wamekuwa wakimpa sapoti kwenye muziki wake.

“Kama unavyoona hapa bajaji na bodaboda zote zina picha yangu, huu ni upendo mkubwa sana, ndiyo maana nikaona kwa kidogo nilichojaliwa nigawe mafuta na niweke saini yangu kama shukrani,” alisema memba huyo wa WCB.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*