googleAds

RAY C AMWONYA LADY JAY DEE

NA CHRISTOPHER MSEKENA

REHEMA Chalamila maarufu Ray C ambaye ni staa wa Bongo Fleva, amemwonya Lady Jay Dee kutorudia tena kufikiria kunywa sumu anapokutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Ray C alitumia ukurasa wake wa picha juzi kuonyesha kusikitishwa na ujumbe aliouandika Lady Jay Dee wiki iliyopita uliodai alihisi kutaka kunywa sumu.

“Kama kuna mtu aliyetakiwa kufanya hili (kunywa sumu) nadhani mimi ndiyo ningekuwa wa kwanza, kama ni kweli haya maneno umeandika wewe naomba shetani ashindwe kabisa, naelewa umepitia mengi kikazi na kifamilia ila katika watu wabishi ninaowaaminia na kuwaheshimu kwenye hii ‘Industry’ wewe pia umo kwa hiyo tafadhali, usirudie haya maneno tena na yafute kwenye nafsi yako, Mungu hapendi,” aliandika Ray C ambaye yupo nchini Oman.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*