googleAds

RAPA MAREKANI: MIMI NI MNIGERIA

LAGOS, Nigeria

MKALI wa muziki wa hip hop kutoka Marekani, Big Sean, amefichua kuwa ana asili ya Nigeria katika mahojiano yake na jarida la Vibe.

Katika video ya dakika saba ya mahojiano hayo, Big Sean anasikika akisema bibi yake ndiye mzaliwa wa Nigeria ingawa baadaye alihamia Detroit, Michigan, Marekani.

Umaarufu wake katika soko la muziki wa hip hop Marekani, ulianza mwaka 2005 alipotangaza katika kituo kimoja cha redio kwamba anataka mashindano ya ‘freestyle’ na Kanye West.

Baadaye, wawili hao walikutanishwa na Kanye mwenyewe akaukubali uwezo wa Big Sean na ndipo alipompa mkataba katika lebo yake ya GOOD Music.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*