RAMOS AITAKA BALLON D´OR

MADRID, Hispania

BEKI kisiki Sergio Ramos anaamini kuna uwezekano wa kuichukua tuzo ya Ballon d’Or licha ya wengi kuona ni ndoto za kiwendawazimu.

Ramos amedai kwamba ni jambo linalowezekana kwake kushinda tuzo hiyo mbele ya mastaa, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Nyota hao wamekuwa wakipokezana tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka tisa sasa.

Kama alivyofanya beki Fabio Cannavaro mwaka 2006, Ramos hana shaka kwamba siku moja itatua mikononi mwake.

“Ballon d’Or imekuwa ya watu binafsi kati ya Messi and Ronaldo. Lakini, kwa mfano Cannavaro aliyekuwa rafiki yangu, alishinda.

Ni mabeki wanne pekee waliowahi kutwaa tuzo hiyo, ambao ni Beckenbauer, Lothar Matthaus na Matthias Sammer.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*