RAKITIC AFANYIWA UPASUAJI

CATALUNYA, Hispania

KIUNGO wa Barcelona, Ivan Rakitic, amefanyiwa upasuaji wa kidole, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.

Rakitic alipata majeraha hayo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhii ya Roma.

Mtanange huo uliochezwa Jumanne ya wiki hii nchini Italia, uliwashuhudia Baraca wakichezea kichapo cha mabao 3-0, hivyo kung’olewa katika michuano hiyo.

Nyota huyo alifanyiwa upasuaji juzi na taarifa ya klabu imesema ulikwenda vizuri.

Barca wanaoongoza msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi 11, watashuka dimbani kesho kumenyana na Valencia.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*