googleAds

PONGEZI ZA BASATA ZAMSHTUA NEY WA MITEGO

NA CHRISTOPHER MSEKENA

RAPA anayefanya vyema kwenye Bongo Fleva, Emmnanuel Eribariki ‘Ney wa Mitego’, amesema pongezi alizopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), siku chache baada ya kutoa wimbo wa Alisema, zilimshtua.

Ney wa Mitego ameliambia Papaso la Burudani kuwa, alishtuka kupokea simu kutoka kwa viongozi wa baraza hilo kwani mara nyingi wamekuwa wakimtafuta wanapotaka kufungia nyimbo zake, lakini safari hii ilikuwa tofauti.

“Nawashukuru Basata kwa kupokea vizuri wimbo wangu kiasi cha kunipongeza, nilipopigiwa simu niende ofisini kwao nilishtuka nikajua kimeshanuka huko, naenda kufungiwa lakini nilipofika hali ilikuwa tofauti walinipongeza kwa kutoa kazi nzuri,” alisema Ney wa Mitego.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*