googleAds

Pointi za Simba zaitoa udenda Lipuli FC

NA WINFRIDA MTOI

KITENDO cha Simba kuendelea kutawala katika Ligi Kuu Tanzania Bara, kimewatamanisha Lipuli FC wanaopambana kukaa kileleni mwa Ligi hiyo.
Lipuli iliwahi kukaa kileleni msimu huu baada ya kushinda mechi ya kwanza ya ligi ikiifunga Mtibwa Sugar mabao 3-0, ikiwa timu yakwanza kutoa kichapo kikubwa.


Kwa sasa Simba ndiyo inashikilia usukani wa ligi ikiwa na pointi 12, ilizokusanya katika michezo minne waliyocheza.
Akizungumza na DIMBA, Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Herman Haruna, alisema, walitamani kukaa kileleni mwa ligi bila kushuka lakini kupoteza pointi nne za michezo miwili waliyotoka sare kuliwagharimu.


Alisema waliposhinda mechi mbili za kwanza, waliweka mipango ya kuendelea kutoa vichapo, ila mambo yakaenda tofauti na matokeo yake michezo miwili ya mwisho wakaambulia sare.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*