googleAds

Pogba, Sanchez wachafua hali ya hewa Man Utd

LONDON, England

MASTAA Paul Pogba na Alexis Sanchez, wanadaiwa kuwa chanzo cha kuzuka mgawanyiko kwenye vyumba vya kubadilishia jezi vya Manchester United, kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho wanalipwa wanapofunga bao na kutoa ‘asisiti’.

Wawili hao wanadaiwa kuwa na mikataba minono katika klabu hiyo ya  Manchester United na ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Sanchez anaripotiwa kulipwa pauni 500,000 kwa wiki na huku akivuta pauni 75,000 kwa kila bao analofunga na huku akikinga tena kitita cha pauni 25,000 kwa kila ‘asisiti’.

Gazeti hilo liliripoti kwa wakati staa huyo akikinga kiasi hicho huku mwenzake Pogba yeye anaingiza pauni 50,000 kwa kila bao na huku akivuta pauni 20,000 kwa kila ‘asisiti’.

Gazeti hilo liliripoti kuwa licha ya kutolewa fedha kwa kila bao, ni jambo la kawaida kwa klabu lakini kiasi wanachokinga mastaa hao ni kikubwa mno kiasi cha kuzua mpasuko kati yao na wachezaji wengine ndani ya vyumba hivyo vya kubadilisha jezi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*