Pochettino: Wachezaji wangu ni mashujaa

LONDON, England

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema wachezaji wake ni mashujaa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao ya ugenini dhidi ya Man City na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Spurs iliivaa Man City usiku wa kuamkia jana, lakini licha ya kutandikwa mabao 4-3, walifanikiwa kuing’oa City kwenye Ligi ya Mabingwa kwa sheria ya bao la ugenini kutokana na kushinda mechi ya nyumbani bao 1-0.

Kichapo hicho kilikamilisha misimu mitatu mfululizo ambayo imeshuhudiwa Man City ya Pep Guardiola ikishindwa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nina furaha. Najivunia kupita kiasi kutimiza ndoto hii ya kucheza nusu fainali. Wachezaji wangu wameonesha ushujaa,” alisema Pochettino.

“Mechi mbili dhidi ya Man City zilikuwa ni kama fainali, lakini tumeonesha upinzani na kushinda. Tumedhihirisha kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*