Pochettino haendi popote

LONDON, England 

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anaamini wachezaji wake wote wapo nyuma yake na ataendelea kukinoa kikosi hicho bila yhofu.

Kauli hiyo aliisema baada ya baadhi ya mastaa wa timu hiyo kumwalika chakula cha usiku katika moja ya mgahawa maarufu jijini London.

“Kila mchezaji alinitumia ujumbe wa mwaliko, hii ni dalili nzuri sana, kujenga umoja na ushikirikano kwenye timu ni jambo la msingi,” alisema Pochettino.

Tottenham haijaanza msimu vizuri na mwenendo wao kwa mechi za hivi karibuni umekuwa mbovu kufanya wachambuzi wengi kumtabiria Pochettino maisha mafupi sema.

Kocha huyo raia wa Argentina ameshinda mechi moja kati ya sita lakini amesisitiza, Tottenham ipo katika kipindi cha mpito.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*