POCHETTINO ANA HOFU SANA

LONDON, England


KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema ana wasiwasi na kikosi chake kufanya vizuri msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 na Girona katika mchezo wa kirafiki.

Pochettino atawakosa nyota wake waliokuwa katika vikosi vya timu za Taifa kama Harry Kane, Hugo Lloris, Delle Ali na wengine wengi.

“Nafurahi tumemaliza michezo yetu ya kujiandaa na msimu lakini michezo ya kwanza ya ligi nitawakosa wachezaji wangu tegemeo,” alisema kocha huyo.

Tottenham watafungua pazia la Ligi Kuu England kwa kucheza dhidi ya Newcastle United katika Uwanja wa St. James Park.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*