googleAds

Platini chini ya ulinzi, kisa tuhuma za rushwa

PARIS, Ufaransa 

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Michel Platini, ameitwa na kitengo cha kuzuia rushwa cha Ufaransa, ili kufanyiwa uchunguzi baada ya kuipa Qatar, uwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022.

Platini, mwenye umri wa miaka 63, kipindi hicho alikuwa madarakani mwaka 2015, kabla ya kufungiwa baada ya kukiuka maadili ya soka.

Qatar iliyapiku mataifa mbalimbali makubwa, yakiwamo Marekani, Australia, Korea Kusini na Japan, huku kukizuka hofu huenda zilitumika njama ili kupitishwa.

Platini alikamatwa juzi kwaajili ya mahojiano maalumu baada ya kubainika kwa tukio ambalo lilifanyika katika Jiji la Paris, Ufaransa, kabla ya kuachiwa huru.

Akizungumza baada ya kuachiwa huru, Platini alidai aliulizwa maswali mengi kuhusiana na tuhuma hizo.

“Yalikuwa ni maswali mengi na yalichukua muda mrefu kujibu na sikuacha hata moja, nilijibu yote, mengine yalihusu Kombe la Dunia la mwaka 2016,” alisema Platini.

Ilielezwa kuwa sakata hilo lilikuwa likifuatiliwa na kufanyiwa uchunguzi kwa muda wa miaka miwili ambayo lilihusiana pia na fainali za Kombe la Dunia za mwaka jana yaliyofanyika Ufaransa.

Taarifa ziliripoti kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter, naye aliwahi kuhojiwa mwaka 2017, kuhusiana na tuhuma kama hizo.

Hata hivyo, Platini alikana tuhuma hizo na kudai kuwa hahusiki na yupo tayari kukabiliana na maamuzi yoyote ambayo yatajitokeza baada ya mahojiano hayo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*