Guardiola na mwanzo wa kuvutia ndani ya Man City

MANCHESTER, England ALIPOTUA Manchester, macho na masikio ya wadau wengi wa soka walisubiri kumwona akidhihirisha ubora wake katika suala zima la ufundishaji soka tangu alipoanza na Barcelona hadi kuelekea Bayern Munich. Na sasa akiwa na kikosi cha Manchester City, Pep Guardiola anafurahia kuanza kwa kasi ya hali ya juu iliyomfanya awe na mwanzo mzuri zaidi ndani ya viunga vya jiji […]

D’banj ametoswa lebo ya Kanye West?

LAGOS, Nigeria MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa Nigeria, D’banj, ameelezwa kusitishiwa mkataba wake na lebo ya muziki ya G.O.O.D Music, inayomilikiwa na staa wa muziki wa hip hop kutoka Marekani, Kanye West. Kilichozua shaka kuwa huenda D’banj ametemwa ni kitendo cha lebo hiyo kutoa orodha ya majina ya wanamuziki wao, huku lile la nyota huyo likikosekana. Kwa mujibu wa orodha hiyo, […]

Aachana na demu wake kisa Wizkid

LAGOS, Nigeria RAPA anayetikisa vilivyo kwenye soko la muziki la Nigeria, Skales, amebwagana na mpenzi wake, huku sababu ya kufikia uamuzi huo ikitajwa kuwa ni msichana huyo kumpenda staa Wizkid. Baada ya kuachana na mchumba wake huyo, imedaiwa kuwa Skales ameamua kutoka na kidosho mmoja kutoka pande za Ethiopia. Wizkid na Skales wamekuwa kwenye vita ya maneno tangu mwaka 2015 […]

Suker: Modric ndiye kiungo bora duniani

MADRID, Hispania UNAMKUMBUKA mpachikaji mabao wa zamani wa Arsenal, Davor Suker? Kwa uzoefu wake, Luka Modric wa Real Madrid ndiye kiungo bora kuliko wote duniani. Suker, ambaye aliwahi pia kukipiga Madrid, kwa sasa ni rais wa Shirikisho la Soka la nchini kwao Croatian. “Si rahisi (kusema Modric ni bora duniani) kwa sababu kuna Cristiano (Ronaldo), (Lionel) Messi, Neymar, Luis Suarez… […]

Unajua kwamba Man City, Uefa ni chui na paka?

MANCHESTER, England MANCHESTER City inajaribu kuangalia uwezekano wa kujenga utawala wao wa soka barani Ulaya, hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Msimu uliopita, wakiwa chini ya kocha Manuel Pellegrini, safari ya Man City katika michuano hiyo iliishia hatua ya robo fainali. Mabingwa wa soka wa La Liga, Real Madrid, ndio waliozika ndoto ya timu hiyo kutinga nusu fainali […]

Klopp: Mkizidi kunifurahisha nitawakumbatia mpaka basi

MERSEYSIDE, Liverpool KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amewapasha wachezaji wake kwa kuwaambia kwamba kama wanataka kuuona upendo wake kwao, basi hawana budi kupambana uwanjani na kumpa raha. Bosi huyo wa majogoo hao wa jiji alionekana ni mwenye Furaha, huku akiwakumbatia wachezaji wake mara baada ya kumaliza mchezo wao wa ligi dhidi ya Chelsea kwa ushindi wa mabao 2-1. […]

Conte amtaja mchawi wake Chelsea

LONDON, England KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amefunguka na kusema kwamba kiungo wake, Cesc Fabregas, ndiye anayempa tabu ndani ya kikosi hicho hadi sasa. Conte hakumpanga Mhispania huyo kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza mtanange wa ufunguzi wa Ligi Kuu England, na amekiri kuwa alipata wakati mgumu wa kumpanga kwenye kikosi cha kwanza kilichofungwa mabao 2-1 na Liverpool […]

Torres: Huu ni wakati mzuri wa kupambana na Barcelona

MADRID, Hispania MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya Atletico Madrid, Fernando Torres, ameweka wazi morali ya hali ya juu aliyonayo kwa kusema kuwa, wakati huu ndio mzuri kupambana na Barcelona kwenye mtanange wao wa La Liga wiki hii. Torres aliiongoza Madrid kuinyuka klabu ya Sporting Gijon mabao 5-0, huku wapinzani wao watakaokutana nao mapema wiki hii, Barca wakiitandika Leganes mabao 5-1 […]

Man United wachapwa mechi ya tatu mfululizo

LONDON, England Manchester United wamepoteza mechi yao ya tatu mfululizo, baada ya kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana. Etienne Capoue alifunga bao lake la nne msimu huu katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Vicarage Road, kabla ya Marcus Rashford kusawazisha baada ya mapumziko. Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Walter Mazzarri ya kumwingiza Juan […]

Shearer aivulia kofia Arsenal

LONDON, England ALAN Shearer ameisifia Arsenal baada ya kuichapa Hull City kwenye mchezo wa Jumamosi ya wiki iliyopita. Gunners walishinda mabao 4-1 kwenye Uwanja wa KC dhidi ya kikosi ambacho mchezaji wao, Jake Livermore alitolewa kwa kadi nyekundu. Lakini Shearer alisema kadi nyekundu imeleta mabadiliko madogo kwenye matokeo. Akiwa kama mchambuzi wa mechi hiyo kwenye moja ya vituo vya televisheni […]