Ni vita Ngoma, Mwanjali Oktoba mosi

NA ZAITUNI KIBWANA ZIKIWA zimebaki siku chache ili tuweze kuona pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, homa ya pambano hilo inazidi kupanda kila kukicha. Ni mechi ambayo inavuta hisia za mashabiki na watu wengine kwa ujumla ambapo kwa mwaka huu kila timu inaonekana kujipanga kisawasawa kwa ajili ya kuibuka kidedea kwenye mchezo huo. Kuelekea mchezo huo utakaochezwa Oktoba […]

Yanga yapanga Vituo vitatu vya mauaji ya Simba

NA MWANDISHI WETU BAADA ya tambo kibao, Oktoba mosi ndiyo siku ya hukumu na mbabe kati ya Yanga na Simba atafahamika siku hiyo pale kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kuelekea kwenye pambano hilo tayari Yanga imepanga vituo vitatu vya mauaji ya watani wao wa jadi, Simba ambao msimu huu wanaonekana kujiimarisha zaidi ya msimu uliopita. Vituo hivyo […]

Pambano la Mayweather, McGregor hakijaeleweka

BONDIA Floyd Mayweather, ameachana na mpango wake wa kuhangaikia pambano lake na Conor McGregor. ‘Money’ ambaye Septemba 2015 alimdunda kwa pointi Andre Berto, alitajwa kuingia ulingoni kuzichapa na mshkaji huyo mwaka huu. Kwa upande wake, Mayweather amedai kuwa McGregor ni mwanamasumbwi pekee ambaye hajawahi kurudiana naye. “Nilijaribu kufanya pambano liwezekane kati yangu na Conor McGregor,” alisema  Mayweather alipokuwa akihojiwa na […]

Wakala: Nani kasema Gotze alichemsha Bayern?

MUNICH, Ujerumani WAKALA wa staa, Mario Gotze, Roland Eitel, amewakosoa wanaosema kuwa kiungo mshambuliaji huyo hakufeli katika misimu yake mitatu aliyocheza Bayern Munich kabla ya kurejea Borussia Dortmund. Mwaka 2013, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alijiunga na Bayern akitokea Dortmund, lakini hakuonekana akiwa kwenye ubora wake na ndipo alipoamua kujiunga na klabu yake hiyo ya zamani ya Dortmund. Hata […]

Saida Karoli aifagilia ‘Salome’ ya Diamond Platnumz

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU kadhaa baada ya nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Salome uliowahi kuimbwa miaka ya 2000 na msanii Saida Karoli, staa huyo wa nyimbo za asili, amesema wimbo huo umetendewa haki. Akizungumza na Papaso la Burudani, Saida Karoli alisema  hivi sasa amerekodi wimbo unaohusu tetemeko la ardhi lililotokea huko Kagera, […]

Siri ya kuvunjika kwa ndoa ya Angelina Jolie na Brad Pitt

NEW YORK, Marekani MWIGIZAJI maarufu wa kike, Angelina Jolie, amefungua kesi ya kudai talaka baada ya kutengana na mumewe, Brad Pitt, ambaye pia ni mwigizaji. Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa miaka 12, kabla ya kufunga ndoa miaka miwili iliyopita. Nyota huyo mwenye miaka 41, Angelina ambaye alikataa kupatanishwa na kuamua kuvunja ndoa yao akidai kwamba hafurahishwi jinsi Brad anavyoishi […]

Messi, Suarez, Griezmann na vita ya Pichichi

MADRID, Hispania VITA ya kuwania tuzo ya ufungaji bora (Pichichi) Ligi ya La Liga tayari imeanza kwa nyota watatu kuanza makeke mapema nchini Hispania. Washambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, Luis Suarez na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid wameanza kufanya kweli na jana usiku walitarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa Camp Nou. Katika mechi zao nne pekee, nyota hao tayari wamejikusanyia mabao […]

Siri ya mabao ya Marcus Rashford

MANCHESTER, England Marcus Rashford ameweka wazi siri iliyojificha nyuma ya mabao yake katika kikosi hicho cha Manchester United. Rashford amefunga mabao 10 katika mechi 23 tangu alipoanza kwenye kikosi cha wakubwa na kufunga mabao mawili dhidi ya Midtjylland katika msimu uliopita wa Ligi ya Europa. Mabao yake yote msimu huu ameyafunga akiwa umbali mdogo na goli, bao lake la kwanza […]