Acha kujifikiria mwenyewe, mapenzi ni yenu wote

MAPENZI ni suala linalohitaji kila mmoja ajitoe kwa mwenzake ili ile raha na amani tarajiwa iweze kupatikana. Ukiwa katika mahusiano suala la kujiangalia wewe tu inabidi likome. Sasa baada ya kuamua kuingia katika maisha ya ndoa zile habari za safari zisizoeleweka inabidi zisiwepo tena. Yale mambo ya kufanya huku ukijiangalia wewe tu pia ni lazima yaishe, ikiwa unataka mahusiano yako […]

Mastaa hawa wamepikwa La Masia

CATALUNYA, Hispania KUNA kipindi bosi wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu, aliwahi kuijia juu FIFA  akipinga uamuzi wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni wa kuiadhibu klabu yake kusajili, akisema  ni uonevu. Kwa mujibu wa FIFA, Barca walivunja taratibu za usajili wa wachezaji wenye umri mdogo. “Ningependa kuweka wazi kuwa Barca wanakubaliana na sheria za FIFA kuhusu usajili wa wachezaji chipukizi,” […]

Kolabo ya Weusi, Sauti Sol ni zaidi ya Gere

NA CHRISTOPHER MSEKENA, BAADA ya kutikisa chati za muziki Afrika kupitia wimbo wao unaoitwa Gere, kundi la Weusi, linaloundwa Joh Makini, Nikki wa Pili na G Nako, limewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wa ngoma yao mpya waliyowashirikisha Sauti Sol kutoka Kenya. Alizungumza na Papaso la Burudani, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Joh Makini, alisema kuwa ni miezi […]

Jux kutumia ‘mic’ yake binafsi

NA ESTHER GEORGE, KATIKA kufanya mabadiliko ya muziki wake, staa wa singo ya Wivu, Juma Mussa ‘Jux’, amesema hivi sasa kwenye maonyesho atakuwa anatumia kipaza sauti ‘mic’ yake binafsi tofauti na zile zinazowekwa jukwaani. Jux ameliambia Papaso la Burudani kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwa tofauti na wasanii wengine na mabadiliko hayo yataendelea sehemu nyingine mbali na kutumia kipaza sauti […]

Umemsikia Wijnaldum wa Liver?

MERSEYSIDE, England STAA mpya wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, ni kama amewatisha mashabiki wa timu pinzani, akiwaambia kocha wake, Jurgen Klopp, anajipanga kufanya mambo makubwa klabuni hapo. “Ni kikosi chenye vipaji na kocha bora,” alisema Wijnaldum na kuongeza: “Naamini kuna kitu anajaribu kukijenga. Nilihisi hivyo siku ya kwanza kukutana na Jurgen Klopp.” Kiungo huyo raia wa Uholanzi, alitua Anfield siku chache […]

Guardiola na mwanzo wa kuvutia ndani ya Man City

MANCHESTER, England ALIPOTUA Manchester, macho na masikio ya wadau wengi wa soka walisubiri kumwona akidhihirisha ubora wake katika suala zima la ufundishaji soka tangu alipoanza na Barcelona hadi kuelekea Bayern Munich. Na sasa akiwa na kikosi cha Manchester City, Pep Guardiola anafurahia kuanza kwa kasi ya hali ya juu iliyomfanya awe na mwanzo mzuri zaidi ndani ya viunga vya jiji […]

D’banj ametoswa lebo ya Kanye West?

LAGOS, Nigeria MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa Nigeria, D’banj, ameelezwa kusitishiwa mkataba wake na lebo ya muziki ya G.O.O.D Music, inayomilikiwa na staa wa muziki wa hip hop kutoka Marekani, Kanye West. Kilichozua shaka kuwa huenda D’banj ametemwa ni kitendo cha lebo hiyo kutoa orodha ya majina ya wanamuziki wao, huku lile la nyota huyo likikosekana. Kwa mujibu wa orodha hiyo, […]

Aachana na demu wake kisa Wizkid

LAGOS, Nigeria RAPA anayetikisa vilivyo kwenye soko la muziki la Nigeria, Skales, amebwagana na mpenzi wake, huku sababu ya kufikia uamuzi huo ikitajwa kuwa ni msichana huyo kumpenda staa Wizkid. Baada ya kuachana na mchumba wake huyo, imedaiwa kuwa Skales ameamua kutoka na kidosho mmoja kutoka pande za Ethiopia. Wizkid na Skales wamekuwa kwenye vita ya maneno tangu mwaka 2015 […]

Suker: Modric ndiye kiungo bora duniani

MADRID, Hispania UNAMKUMBUKA mpachikaji mabao wa zamani wa Arsenal, Davor Suker? Kwa uzoefu wake, Luka Modric wa Real Madrid ndiye kiungo bora kuliko wote duniani. Suker, ambaye aliwahi pia kukipiga Madrid, kwa sasa ni rais wa Shirikisho la Soka la nchini kwao Croatian. “Si rahisi (kusema Modric ni bora duniani) kwa sababu kuna Cristiano (Ronaldo), (Lionel) Messi, Neymar, Luis Suarez… […]