Kally Ongala mambo freshi Majimaji

NA GEORGE KAYALA KOCHA Kally Ongala, amekubali kurejea kuifundisha timu ya Majimaji ya Songea inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Kocha huyo aliikacha timu hiyo aliyoifundisha mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita baada ya kukumbwa na ukata, hivyo kuhofia mustakabali wa mshahara wake. Ongala alisema tayari ameshafanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo na kuwapa masharti kuhusiana na […]

Kiiza katika kibarua kigumu Sauzi leo

NA MWANDISHI WETU MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba Mganda, Hamis Kiiza, leo ndiyo kipimo cha uwezo wake kitakapoonekana kikosi chake cha Free State kitakapoikabili timu ngumu ya SuperSport United. Kikosi hicho cha Free State Stars kitakuwa ugenini katika Uwanja wa King Zwelithini Stadium, dhidi ya wapinzani wao hao ambapo Kiiza anatarajiwa kuonyesha uwezo wake ili kudhihirisha kuwa hakusajiliwa kwa bahati […]

Genk ya Samatta yapiga mtu 4-0

NA MWANDISHI WETU BAADA ya kupokea vipigo vitatu mfululizo, hatimaye kikosi cha Genk kinachoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, kimefufuka na kuifunga  Eandracht Aalst. Kikosi hicho kiliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mchezo wa Kombe la Ligi ambao hata hivyo Samatta hakuwepo kutokana na maumivu ya goti yanayomkabili. Mpaka sasa nahodha huyo wa timu ya Taifa ya […]

Simba Ukawa: Tukirudishwa kundini Yanga wamekwisha

NA EZEKIEL TENDWA UNALIKUMBUKA lile kundi la Simba Ukawa? Sasa limeibuka na kusema kuwa Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva, hajatoa kauli ya kuwarudisha kundini na kama atafanya hivyo kabla ya mchezo dhidi ya Yanga, Wanajangwani hao watalia kilio kikubwa. Simba na Yanga zinakutana Oktoba mosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo kundi hilo la Simba Ukawa limesema […]

SIMBA VS YANGA OKT MOSI  NI SHOO YA KICHUYA NA MAHADHI

NA ZAITUNI KIBWANA KUELEKEA mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, homa ya pambano hilo imezidi kupanda baada ya kila timu kumtambia mwenzake. Zikiwa ni siku chache kabla ya mchezo huo utakaochezwa Oktoba Mosi, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuna mambo mbalimbali ya kuyaangalia, lakini leo tukiwatupia macho winga wa Simba, Shiza Kichuya na yule wa […]

Micho awakutanisha Vincent Bossou, Jjuuko

NA ZAITUNI KIBWANA KOCHA wa timu ya Taifa ya Uganda ‘Cranes’, Milutin Sredojevic ‘Micho’, amemkutanisha beki wa Simba, Jjuuko Murushid na kisiki cha Yanga, Vincent Bossou, kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya Uganda na Togo. Mchezo huo unaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), umepangwa kuchezwa Oktoba 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kegue, mjini Lome, Togo. […]

Jonas Mkude awapa habari njema Msimbazi

NA HUSSEIN OMAR NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amewatoa hofu mashabiki wa timu  hiyo akiwataka kujitokeza kwa wingi Oktoba Mosi, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kushuhudia jinsi watakavyoisambaratisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakitamba kuendeleza ubabe wao kwa Simba, kama walivyofanya msimu uliopita pale waliposhinda mechi zote mbili […]