Joe Hart kuwa mrithi wa Courtois Chelsea

LONDON, England TIMU ya Chelsea inasemekana kumfukuzia mlinda mlango wa Manchester City, ambaye anakipiga kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Torino, Joe Hart, ili aweze kuwa mrithi wa nyota wao, Thibaut Courtois. Hatua hiyo ya Chelsea inasemekana kuja baada ya Courtois kuendelea na msimamo wake wa kuwa na ndoto za kutaka kurejea nchini Hispania. Gazeti la The Sun […]

Guardiola kuwapiga panga Aguero, Kompany

LONDON, England KOCHA  wa Manchester City, Pep Guardiola, anasemekana kuwa na mpango wa kuwapiga panga mastaa wake wawili, Sergio Aguero na  Vincent Kompany, wakati wa usajili wa majira ya joto yajayo. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya klabu hiyo vinaeleza kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa kocha huyo kutaka kukijenga upya kikosi chake kwa kuwatumia wachezaji ambao anawahitaji.

Mkhitaryan Kinachomtesa Old Trafford ni historia yake mwenyewe

MANCHESTER, England MIONGONI mwa mastaa ambao usajili wao uliteka vichwa vya habari wakati wa majira ya kiangazi ni Henrikh Mkhitaryan. Akitokea Borussia Dormund ya Bunderliga, kiungo huyo wa pembeni alitua Old Trafforrd kwa ada inayotajwa kuwa ni zaidi ya pauni milioni 20. Kilichowashitua wengi si kiasi hicho kikubwa cha fedha, bali kipaji cha hali ya juu alichonacho staa huyo. Kwa […]

Mkutano wa kesho usigeuzwe sehemu ya kukomoana

NA MWANDISHI WETU, MAPENZI kwa mtu au kitu ni gharama kubwa kwa anayependa. Huna ujanja kwa vile utaingia hiyo gharama. Kesho, wanachama wa Yanga wanakwenda katika mkutano wa dharura ambao umeitishwa na uongozi wao na utafanyika kwenye makao makuu ya klabu yao katika mitaa ya Twiga na Jangwani, eneo la Kariakoo, mjini Dar es Salaam. Tayari ajenda za mkutano huo […]

Wanatakiwa kutafakari na kuchukua hatua

NA ZAINAB IDDY, UMEBAKI mwezi mmoja na wiki chache kabla ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17 kumalizika. Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa Desemba 15 itakuwa siku rasmi ya kuanza kwa usajili wa dirisha dogo. Ni kipindi ambacho klabu za Ligi Kuu hukitumia kurekebisha kasoro mbalimbali, ikiwemo kusajili wachezaji wapya, zoezi ambalo […]

Waamuzi wabovu kichaka cha mapungufu ya timu zetu

NA MWANDISHI WETU, FEBRUARI 13, 1960 katika mji wa Bologna nchini Italia, alizaliwa mwanadamu aliyeaminika ndiye refa bora kabisa wa soka wa kizazi chake. Huyu si mwingine bali ni Peirluigi Collina. Alikuwa na sura ya majukumu na macho ya kukera ya ‘paka’ yaliyomfanya aweze kuuona mpira mara nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote pale uwanjani. Refa huyu bora wa karne […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [24]

Ilipoishia jana Aliamua kulelekea kwenye lifti ambapo aliingia na kubonyeza kitufe namba sifuri, akitaka kwenda chini kwanza kabla ya kuelekea ghorofa ya nne ambako kuna chumba chake. Alipofika chini ambako kuna watu wengi, mbele yake aliwaona watu wasiopungua watano, wakitoka nje na kuingia ndani ya hoteli, wakija kwenye lifti. Watu hao aliwaona ni wa tofauti kidogo, kutokana na umakini wao […]

Pogba amvimbisha kichwa Mourinho

LONDON, ENGLAND KWA kile ambacho unaweza kusema ni kamvimbisha kichwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema vyombo vya habari viliwahi mno kuhukumu uwezo wa mchezaji wake, Paul Pogba, aliyejiunga na timu hiyo akitokea timu ya Juventus ya Italia. Mourinho alitoa kauli hiyo juzi mara baada ya staa huyo kuifungia timu yake mabao mawili yaliyoipa ushindi wa 4-1 dhidi ya […]

Ozil amsikilizia Wenger

LONDON, England STRAIKA Mesut Ozil, anamsikilizia kocha wake, Arsene Wenger, kuhusu hatima yake kwenye klabu hiyo kabla ya kusaini mkataba mpya. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya klabu hiyo, Arsenal inataka kumfanya Mjerumani huyo kuwa mmoja kati ya wanaolipwa fedha nyingi, lakini kwanza anachotaka kukifahamu ni kama Wenger ambaye mkataba wake unafikia kikomo Juni mwakani atamwaga wino […]