Kichuya: Ngoma, Chirwa wasubiri sana tu

NA ZAINAB IDDY, WINGA  wa Simba, Shiza Ramadhani  ‘Kichuya’, amesema washambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma na  Obrey Chirwa watasubiri kufikia  idadi ya mabao aliyofunga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Tayari Kichuya amefunga mabao saba kabla ya mechi ya jana dhidi ya Toto Africans, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, huku Ngoma na Chirwa wakifunga […]

Simba yazidi kujikita kileleni

NA ZAITUNI KIBWANA, SIMBA wamepania bwana. Ndivyo unavyoweza kusema, maana kila anayeingia anga zake anapigwa tu. Jana ilikuwa zamu ya Toto Africans ya Mwanza kupokea kipigo chake, ambapo ilipokea kichapo cha mabao 3-0. Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, umeifanya Simba kuendelea kukaa kileleni kwa kufikisha pointi 29, ikiongeza […]

Cannavaro: Pointi tatu nyingine zinakuja

NA SALMA MPELI, NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kuelekea mechi yao dhidi ya JKT Ruvu, inayotarajiwa kupigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Uhuru, wanajipanga kuhakikisha wanachukua pointi tatu nyingine ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao. Akizungumza na BINGWA jana, wakiwa njiani kurejea Dar es Salaa wakitokea mkoani Kagera, Cannavaro alisema, Ligi ni ngumu na kila […]

Akilimali atengua kauli Yanga

NA WINFRIDA MTOI, BAADA ya mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuanza kufunga, Katibu wa Baraza la Wazee wa timu hiyo, Ibrahim Akilimali, ametengua kauli yake aliyowahi kutoa juu ya mchezaji huyo na kusema kuwa hana tatizo naye kwa sasa. Akilimali aliwahi kutoa kauli siku za nyuma kuwa anashangazwa na kitendo cha Yanga kumsajili mchezaji huyo kwa pesa nyingi, wakati […]

Real Madrid kumng’oa Pogba Man Utd

MADRID, Hispania RAIS wa timu ya Real Madrid, Florentino Perez, amethibitisha kuwa wapo kwenye mazungumzo ya kuhakikisha Paul Pogba  anatua katika klabu yake ya Manchester United. Kwa mujibu wa gazeti la Marca, Perez alitoa taarifa hizo juzi, wakati akijibu maswali  na kuelezea hali ya klabu mbele ya washirika na viongozi wa klabu pamoja na wajumbe waliompigia kura rais  huyo wa […]