Asya Idarous alivyofunika Shikamoo Swahili Fest Marekani

NA MWANDISHI WETU, Mkongwe wa mitindo ya mavazi nchini Tanzania, Asya Idarous ‘Mama wa Mitindo’, mwishoni mwa wiki iliyopita alitia fora kwenye onyesho kubwa la mavazi nchini Marekani. Onyesho hilo, lililopewa jina la Shikamoo Swahili Festival, lilifanyika mjini Atlanta, Georgia na mbunifu huyo mkongwe kupata fursa ya kuonyesha mavazi yake ya kitamaduni za Kiswahili. Lengo la onyesho hilo la mavazi […]

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [25]

Ilipoishia Jana Roika hakujibu chochote, alibaki kimya kwa sekunde kadhaa, kitendo kilichozidi kumshtua Ramona. Baadaye kwa moyo wa ujasiri, moyo uliomfanya kusafiri kutoka Mexico kwenda Haiti na baadaye kutoka Haiti kuja Pakistani, ulimtuma kumwambia Ramona kile alichokuwa amekijia Pakistani.  “Ramona nakupenda sana, naomba uje kuwa mke wangu.” SASA ENDELEA Ilionyesha kuwa Ramona alikuwa anajua wazi kama Roika anampenda. Kwani aliposikia […]

Juventus yataka kumchukua bure Thiago Silva

TURIN, Italia MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Italia, klabu ya Juventus, imeonesha dhamira ya kutaka kumchukua mchezaji mwingine mwenye uwezo wa hali ya juu kwa uhamisho wa bure na beki wa PSG, Thiago Silva, yupo kwenye rada za kibibi kizee hicho cha Turin. Silva, mwenye umri wa miaka 32, anatarajiwa kumaliza mkataba wake na mabingwa hao watetezi wa Ufaransa mwishoni […]

Mourinho: Nimuuze Rooney? Haiwezekani

MANCHESTER, England NAHODHA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, aliwahi kufukuziwa na klabu za China ambapo moja ya timu hiyo iliweka mezani mkataba wenye mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki miezi 10 iliyopita. Kocha wake ndani ya klabu hiyo, Jose Mourinho, amesema hataweza kufikia hatua ya kufikiria suala la kumuuza mshambuliaji wake huyo. “Sitafanya uamuzi huo. Kwa heshima na […]

AY, Dj D Ommy, Diamond, Harmonize wawafuta machozi Watanzania

NA HAPPYGLORY URASSA, BAADA ya nyota 6 wa Bongo Fleva kutoka kapa katika tuzo za MTV MAMAs 2016 zilizofanyika juzi, Johannesburg, Afrika Kusini, wasanii AY, Dj D-Ommy, Diamond Platnumz na Harmonize wameibuka washindi kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA), zilizotolewa usiku wa kuamikia jana huko New Jersey, Marekani. Kabla ya tuzo hizo kutolewa, juzi usiku mastaa wa Bongo […]

Ni hatari kubwa mpenzi wako kuamini kuwa humpendi

KILA binadamu kwa namna yake hujiona yeye ni bora zaidi. Yeyote unayemuona mtaani kwa namna yoyote alivyo kuna mahali hujiona yeye ni bora zaidi. Hii tabia ndiyo humfanya binadamu awe na furaha na kujiona anastahili sana kuishi. Binadamu anayetokwa na sifa hii, ama kwa kufanywa kuamini au kwa kujifanya kuamini kuwa yeye si bora, hupoteza furaha ya maisha na hatimaye […]

Arsenal yakerwa na ‘wanaokalia’ tiketi za msimu

LONDON, England KLABU ya Arsenal imedhamiria kuwapa adhabu mashabiki wao walionunua tiketi za msimu kama watashindwa kuwa na mahudhurio mazuri uwanjani baada ya kuumizwa na suala la siti za uwanja wa Emirates kuwa tupu, huku tiketi nyingi zikiwa hazijatumika na mashabiki wao au hata kuziachia kupitia mfumo maalum wa mabadiliko wa klabu hiyo. Na leo Jumatatu, bodi ya Arsenal itakaa […]