Arsenal yazidi kuwang’ang’ania Ozil, Sanchez

LONDON, ENGLAND KLABU ya Arsenal imesisitiza kuwa wana uwezo wa kuwabakiza kundini nyota wao, Mesut Ozil na Alexis Sanchez. Wawili hao wanatarajiwa kumaliza mikataba yao mwaka 2018 na wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kuondoka Emirates. Arsenal walikuwa na utaratibu wa kuwauza wachezaji wao wa kiwango cha juu miaka iliyopita ili kubalasi vitabu vyao vya hesabu. Lakini Ivan Gazidis anaamini Washika […]

Jose Mourinho awapigia magoti mashabiki Man Utd

LONDON, ENGLAND JOSE Mourinho amewaomba radhi mashabiki wa Manchester United kutokana na kipigo cha mabao 4-0 walichokipata kutoka kwa Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England, uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, jijini London. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Mreno huyo alisema kikosi chake kilikumbana na kipigo hicho kutokana na makosa ya […]

Straika Toto African aibua tuhuma nzito

NA WINFRIDA MTOI, MSHAMBULIAJI wa Toto African, Waziri Junior amesema mchawi mkubwa wa timu yao ni kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho. Akizungumza na BINGWA jana, Junior alisema kikosi chao kimekuwa kikishindwa kutengeneza nafasi hatua inayosababisha kukosa ushindi katika mechi mbalimbali za ligi kuu msimu huu. Alisema yeye binafsi anaamini bado anao uwezo mkubwa wa kupachika mabao […]

Ngassa apigwa marufuku kukanyaga Yanga

NA ZAINAB IDDY, BABA mzazi wa winga wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Fanja FC ya Oman, Mrisho Ngassa, Khalfan Ngassa, amesema hategemei mwanawe huyo kurejea kwa mara nyingine katika kikosi cha Yanga. Ngassa alijiunga na Fanja inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Asia siku chache baada ya klabu ya Free State ya Afrika Kusini aliyokuwa anaichezea kusitisha mkataba wake. […]

Muzamiru, Mo Ibrahim wamtikisa Kichuya

NA ZAITUNI KIBWANA, KASI ya viungo wa Simba, Mohammed Ibrahim na Muzamiru Yassin kwenye kikosi cha timu hiyo, imeonekana kumtikisa straika machachari, Shiza Ramadhani ‘Kichuya’. Kichuya ambaye kwa sasa ana mabao saba na kuongoza kwenye msimamo wa wafungaji, amejikuta akishindwa kutikisa nyavu za timu pinzani kwenye mechi ya pili sasa. Winga huyo aliyesajiliwa kutoka Mtibwa kwenye mechi mbili za Toto […]

Malinzi atajwa bao 6 za Yanga

NA EZEKIEL TENDWA, KIPIGO cha mabao 6-2 walichokipata Kagera Sugar kutoka kwa Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera, kinatajwa kuchangiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi. Kagera Sugar ambao mara kwa mara wamekuwa wakitoa upinzani mkubwa wanapokutana na timu kubwa za Simba na Yanga, hasa wanapokuwa uwanja wao huo wa nyumbani, […]

Simba yajibu mapigo Yanga

WINFRIDA MTOI NA SALMA MPELI, BAADA ya Shiza Kichuya kuongoza kwenye orodha ya wafungaji na kwenye klabu yake ya Simba kuonekana kuwa ni tegemeo namba moja, kuliibuka maneno mengi kutoka kwa mashabiki wa Yanga wakidai watani wao wanamtegemea mchezaji huyo pekee kwenye suala zima la ufungaji. Katika kuwadhihirishia watani wao kuwa wanachokisema hakina mashiko, ni kuwajibu kwa vitendo kwenye michezo […]

Lwandamina apewa masharti magumu

NA HUSSEIN OMAR, KATIKA kuhakikisha Yanga inakuwa moto wa kuotea mbali kwenye mechi za kitaifa na kimataifa, uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa mkataba wa miaka miwili, Mzambia George Lwandamina na ndiye atakayechukua nafasi ya Kocha Hans van der Pluijm. Yanga imefikia uamuzi huo baada ya kuona timu yao ikiwa imeshuka kiwango na hivyo kuhofia huenda wakashindwa kutetea taji lao […]

Yanga yanasa beki wa kushoto hatari

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY, HATIMAYE tatizo la beki wa kushoto linaloonekana kuikabili Yanga, linakaribia kupata tiba baada ya uongozi wa timu hiyo kuanza mazungumzo na Ayo Oluwafemi anayekipiga katika kikosi cha Zesco. Ikumbukwe BINGWA lilikuwa gazeti la kwanza kuwajulisha wapenzi wa soka Tanzania kuwa Yanga imemnasa kocha wa Zesco, George Lwandamina, kabla ya wengine ‘kudandia treni kwa mbele’ na […]