Rashford apiga bao tamu ugenini

LONDON, England KOCHA Ole Gunnar Solskjaer ameendelea kuonesha uwezo wake tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa Man Utd, baada ya kuiongoza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, na kufikisha mechi 10 bila kupoteza. Bao pekee la Man Utd lilipachikwa na straika, Marcus Rashford, katika dakika ya tisa ya mchezo huo, baada ya kuipokea pasi iliyopigwa kiufundi na kiungo, […]

Mbelgiji atupiwa lawama

ZAITUNI KIBWANA NA SAADA SALIM MAKOCHA na wachambuzi wa soka, wamemtupia lawama kocha wa Simba, Patrick Aussems, wakieleza mfumo mbovu unaotumiwa na kocha huyo utaendelea kuigharimu timu hata katika mechi za marudiano watakazocheza nyumbani. Simba juzi usiku ilikubali kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Al Alhly ya Misri katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika. Idadi kama hiyo […]

Amri Said angetumia busara kwa kipa wake

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya mechi ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Yanga na Biashara United, kitu kilichozua gumzo kubwa ni kitendo cha Kocha wa Biashara, Amri Said, kuonekana akirushiana maneno na mlinda mlango wake, Nurdin Balora, baada ya kumfanyia mabadiliko. Mlinda mlango huyo alipofika katika benchi baada ya kupumzishwa alionekana kuanza kurushiana maneno na Amri, ambaye aliamua […]

Mgunda kuitolea macho Yanga

NA OSCAR ASSENGA, TANGA KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda, amesema watahakikisha wanapambana kufa au kupona ili kuibuka na ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Yanga na kupanda nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo. Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara inatarajia kuchezwa kesho Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku kocha huyo akitamba kutembeza mkong’oto kwa wana […]

Amunike aula CAF

NA FAUDHIA RAMADHANI SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF), limemteua kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike, kwenye kamati inayohusu masuala ya utafiti ya kiufundi ya michuano ya Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 20. Akizungumzia uteuzi huo, Amunike alisema anajivunia kupewa nafasi hiyo.    “Ni jambo jema kuaminiwa na kuwa miongoni mwa watafiti wa […]

Dante hajashuka

NA MWAMVITA MTANDA BEKI wa timu ya Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’, amesema haikuwa dhamira yake kusababisha penalti katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Biashara United juzi, akieleza mchezo hautabiriki na chochote kinaweza kutokea uwanjani. Dante alisababisha penalti hiyo dakika ya tano ya mchezo huo uliochezwa Uwanja Taifa, Dar es Salaam na kuwafanya Biashara wapate bao la […]

AUSSEMS AMTAJA ANAYEMPA JEURI SIMBA

NA SAADA SALIM KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema amefurahishwa na kitendo cha kurejea kwa mshambuliaji wake, John Bocco, akikiri straika huyo kumpa jeuri kuelekea mechi yao dhidi ya Al Ahly ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Borg El Arab, mjini Alexandria, Misri. Bocco aliukosa mchezo uliopita wa michuano hiyo dhidi ya AS Vita ya […]

Yondani ashtukiwa Yanga

NA HUSSEIN OMAR YONDANI si bure kuna kitu. Hivyo ndivyo wasemavyo baadhi ya mashabiki wa Yanga, wakimwelezea beki wao wa kati, Kelvin Yondani ambaye wanaamini kuna kitu nyuma ya pazia kutokana na kile wanachodai kushuka kwa kiwango chake, tangu alipovuliwa unahodha wa timu hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajib. Katika mechi tatu za Yanga za hivi karibuni dhidi […]