Madee amtolea povu Pogba

NA GRAY PAUL (TUDARCO) RAPA kutoka Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’, jana aliwashangaza mashabiki zake mara baada ya kutoa maneno yaliyozua mjadala kuhusu mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba. Madee alitoa maneno hayo baada ya Manchester United kupoteza mchezo wa tatu mfululizo na kiungo huyo ghali aliyevunja rekodi ya usajili wa pauni milioni 89 akitokea Juventus na kuandika maneno […]

Rodriguez: Namuiga Zidane

MADRID, Hispania NYOTA wa Real Madrid, James Rodriguez, amemmiminia sifa kocha wake, Zinedine Zidane, akisema ndiye kiigizo chake. Mshambuliaji huyo aliyasema hayo baada ya kurudi katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa kuipa Madrid ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Espanyol. Rodriguez ndiye aliyeanza kuziona nyavu za Espanyol katika kipindi cha kwanza, huku bao la pili likifungwa na Mfaransa, Karim Benzema.

Guardiola aanza ‘kujishaua’

MANCHESTER, England   ETI kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amekasirika kwa kuambiwa timu yake itachukua mataji mengi msimu huu. Man City wanaongoza ligi wakiwa na jumla ya mabao 25 na hivi karibuni waliichapa Borussia Monchengladbach mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Guardiola amekataa sifa hizo na kusema kuwa lengo lake kwa sasa ni kuhakikisha mashabiki wa Man […]

Kumbe kipigo kilimpagawisha Pogba!

MANCHESTER, England UNAMKUMBUKA Dirk Kuyt? Ni yule staa wa zamani wa Liverpool ambaye hivi sasa anakipiga Feyenoord? Ameibuka na kusema kuwa Paul Pogba aliwakaripia wachezaji wenzake wa Manchester United, wakati wa mchezo wa wiki iliyopita. Licha ya kusajiliwa kwa dau lililovunja rekodi ya usajili, Pogba hakufurukuta kwa dakika zote 90 huku Man United ikilala kwa bao 1-0. “Nilichokuwa nakisikia kipindi […]

Wenger achimba mkwara mzito

LONDON, England KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kitendo cha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Hull City ni ujumbe tosha kwa wapinzani wake. Kocha huyo amesema matokeo waliyoyapata yanaonesha wazi kuwa timu yake imeiva kupambana kwenye mbio za kufukuzia ubingwa. “Ni ushindi wenye ujumbe,” alisema alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Telegraph. Mpaka sasa Arsenal wameshinda […]

Madrid haikamatiki La Liga

MADRID, Hispania BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa La Liga dhidi ya Espanyol, Real Madrid wameweka rekodi ya kuwa timu iliyoshinda michezo mingi mfululizo. Ushindi huo ni wa 16 mfululizo kwa kikosi hicho kinachonolewa na Mfaransa, Zinedine Zidane ‘Zizou’. Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Barcelona ambayo iliiweka katika msimu wa 2010/11. Katika siku 200 […]

Eti Balotelli atarejea England akiwa mpya!

LONDON, England WAKALA wa straika, Mario Balotelli, Mino Raiola, amesema kwamba mteja wake huyo atarejea tena nchini England mwakani akiwa moto wa kuotea mbali. Kauli ya wakala huyo imekuja ikiwa ni baada ya Balotelli kufufua matumaini ya kurudi kwenye ubora wake baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika mechi zake mbili za mwanzo akiwa na klabu yake mpya ya […]

Mashabiki wataka Mourinho afukuzwe

LONDON, England HALI si shwari kwa kocha, Jose Mourinho, hasa baada ya mwenendo unaoonekana kutowaridhisha mashabiki wa klabu ya Manchester United. Kwa lugha nyepesi na ya kueleweka, kocha huyo ameanza kukumbana na presha ya mashabiki ‘wendawazimu’ wa Old Trafford. Baada ya Sir Alex Ferguson kutundika daluga, David Moyes, alikumbana na presha hiyo kama ilivyokuwa kwa Louis van Gaal ambaye kuondoka […]

Kiiza mzigoni tena kesho Sauzi

NA EZEKIEL TENDWA, BAADA ya kuanza mikikimikiki ya ligi kuu nchini Afrika Kusini kwa kucheza mchezo mwishoni mwa wiki iliyopita, straika wa zamani wa Simba, Hamis Kiiza, kesho anatarajiwa kuonyesha tena makeke yake kwenye kikosi chake cha Free State Stars kitakachowakabili Golden Arrow. Kiiza alianza kuitumikia timu yake hiyo wiki iliyopita walipocheza na Bloemfontein Celtic, mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu […]