PLUIJM: NGOMA NINAYEMJUA MIMI BADO

NA TIMA SIKILO KOCHA Mkuu wa Azam, Hans van der Pluijm, amewaambia mashabiki wa timu hiyo na wengineo kuwa Donald Ngoma wanayemwona sasa, bado hajarudi katika kiwango chake anachokifahamu Mholanzi huyo. Ngoma tangu ameanza kupata nafasi katika kikosi cha Pluijm, ameshacheka na nyavu za wapinzani wao mara tatu na kuhusika kwenye mabao mengine yaliyofungwa na wenzake. Juzi Ngoma alimwezesha Pluijm […]

AUSSEMS AMZIKA RASMI DJUMA

NA ZAITUNI KIBWANA TOFAUTI na ilivyokuwa ikitarajiwa, wapenzi wa Simba tayari wamemsahau aliyekuwa kocha msaidizi wao, Masoud Djuma, kutokana na kandanda safi linaloonyeshwa na kikosi chao chini ya mwalimu Patrick Aussems raia wa Ubelgiji. Tangu vuguvugu la kutimuliwa kwa Djuma kutokana na madai ya utovu wa nidhamu lilipoanza kufukuta ndani ya Simba, wapo wapenzi wa timu hiyo walioamini kikosi chao […]

YANGA: NJOONI TUWAPE RAHA

NA EZEKIEL TENDWA   YANGA wamepata taarifa kwamba watani wao wa jadi, Simba, wamemwangushia mtu kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, hivyo Wanajangwani hao kuapa kuichakaza Lipuli FC leo ili kuendelea kuwapa raha wapenzi wao. Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, waliibuka na ushindi huo mnono dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, […]

MWANAMKE KUWA NA TABIA HII NI HATARI SANA KATIKA MAHUSIANO

NA RAMADHAN MASENGA KIASILI na kitamaduni, mwanaume hupenda kutawala ama kuhisi anatawala. Mwanaume akiona ama akihisi anatawaliwa na mwanamke, hata akiacha kusema hujikuta akianza kujihisi vibaya kuhusu nafsi yake na hatimaye kuhusu huyu mwanamke anayehisi anamtawala. Katika uhusiano wanawake wengi hukosea kwa kuamini, ukali ama kuwa na maneno mengi ya kuudhi ni njia nzuri ya kupambana na wanaume zao katika […]

MMACHINGA ALIINUSURU YANGA KUFUNGWA NA COFFEE 1998

NA HENRY PAUL UNAPOZUNGUMZIA wachezaji wa zamani waliopata mafanikio katika soka, kamwe huwezi kuacha kulitaja jina la mshambuliaji wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’. Mmachinga aliyejiunga na Yanga katika  miaka ya 1990 akitokea Klabu ya Bandari ya Mtwara, ambaye alikuwa mshambuliaji mahiri wa kutegemewa kwa kupachika mabao muhimu katika timu hiyo na kupata mafanikio. Miongoni mwa mafanikio nyota huyo aliyofanya ni […]

JIDE, ZAHARA, KANYOMOZI WAKONGA NYOYO VOCALS NIGHT

NA CHRISTOPHER MSEKENA NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, ameongoza mashabiki wa muziki nchini katika tamasha la Vocals Night lililofanyika kwa mafanikio makubwa mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Tamasha hilo la kila mwaka lenye lengo la kuwainua waimbiaji wa kike nchini, lilikuwa na ugeni mzito wa wanamuziki kama vile staa […]

PATORANKING AKUMBUSHIA VANESSA MDEE KUMLISHA UGALI

NA CHRISTOPHER MSEKENA STAA wa muziki nchini Nigeria, Patrick Okorie ‘Patoranking’, amemtaja msanii Vanessa Mdee kama mtu wa kwanza kumlisha ugali walipokuwa nchini Kenya mwaka jana. Patoranking ambaye mwishoni mwa wiki alifanya bonge la shoo katika kiwanja kipya cha burudani Buckets, Masaki jijini Dar es Salaam, aliliambia Papaso la Burudani kuwa wakati yupo na Vanessa Mdee katika mradi wa Coke […]

MASTAA WAPAMBA MIAKA 20 YA TWANGA PEPETA

NA CHRISTOPHER MSEKENA NYOTA kutoka sekta mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kupamba onyesho maalumu la miaka 20 ya bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, iliyofanyika juzi katika eneo la Life Park, Mwenge, jijini Dar es Salaam juzi. Onyesho hilo lililoanza saa moja jioni kwa wanamuziki na madansa wa Twanga Pepeta kupanda jukwaani wakiwa wamevaa kininja, lilihudhuriwa na wageni wa heshima […]

SIMBA QUEENS YASAJILI VIFAA 12

NA GLORY MLAY TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kusajili wachezaji 12 kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Miongoni mwa wachezaji walionaswa na timu hiyo ni Mwanahamisi Omari, Amina Ramadhan, Amina Ally, Crista John, Rukia Nasri, Zubeda Mohammed, Catherine Shija na Violet Nicholas. Akizungumza na BINGWA jana, kocha mkuu wa […]

PAMBA YAPAA KILELENI FDL

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA MAMBO yamenoga kwa timu ya Pamba ya jijini Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), baada ya kushinda mchezo wake wa tatu mfululizo na kujikita kileleni mwa Kundi B. Katika mchezo uliopigwa juzi Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Wana TP Lindanda Pamba SC, waliichapa Mgambo Shooting ya Tabora 3-0 mabao yaliyofungwa na Ally Athuman dakika […]