Rubby awaacha njiapanda mashabiki

NA BEATRICE KAIZA, MSANII anayefanya vizuri katika tasnia ya Bongo Fleva, Hellen George ‘Rubby’,  amewaacha njiapanda mashabiki wake baada ya kuandika ujumbe katika mitandao wa kijamii wa Instagramu unaoonekana ni fumbo kwao. “Very soon (hivi karibuni) nitaongea vitu ambavyo hakuna mtu anaweza akaamini, ukiona kobe amekaa kimya ujue anatunga sheria,” ulisomeka ujumbe huo. Ujumbe huo umeonekana ni fumbo kubwa kwa […]

Baraka Da Prince ampa onyo Bakora

NA BEATRICE KAIZA, MSANII wa Bongo Fleva nchini, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’, amefunguka na kudai kitendo alichokifanya mchekeshaji, Stan Bakora cha kumwigiza kwenye video yake ya ‘Nisamehe’ hajakipenda na hataki kumwona anakirudia tena. Muda mfupi baada ya Bakora kutuma video hiyo katika mitandao ya kijamii, Baraka alionekana kuchukizwa na hivyo kumwandikia ujumbe uliosomeka kuwa: “Matani ni mazuri ila yakizidi […]

Walcot, tusubiri kuisoma kurasa ya mwisho kwenye kitabu chake

NA ALLY KAMWE, KAMA umepata bahati ya kuitazama Arsenal msimu huu, bila shaka utakuwa umegundua mambo mawili makubwa kutoka kwao. Moja wamepata tiba ya kiungo mkabaji, pili na kubwa zaidi ni Theo Walcot aliyekuwa akisubiriwa tangu Agosti 2006 alipocheza pambano lake la kwanza pale Emirates, ameanza kuonekana. Ndio, kwa miaka 10 mashabiki wa Arsenal wamekuwa kwenye ganzi kubwa wakisubiri kuona […]

Chicharito atakiwa tena La Liga

MADRID, Hispania STRAIKA wa timu ya Bayer Leverkusen, Javier Hernandez maarufu kama Chicharito, anasemekana kuwindwa tena na klabu za Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga. Shirika la Habari nchini humo AS  liliripoti kuwa timu za Valencia na  Sevilla kwa sasa zinapigana vikumbo zikimwania nyota huyo raia wa Mexico ili kuhakikisha zinapata huduma ya nyota huyo wakati wa usajili wa majira ya […]

Wanne watakiwa kuziba pengo la Milik Napoli

ROMA, Italia KLABU ya Napoli inasemekana kuwa na mpango wa kuwanasa mastraika  Emmanuel Adebayor, Dimitar Berbatov, Marouane Chamakh ama Kevin Kuranyi ili mmoja wao aweze kuziba pengo la staa wao, Arkadiusz Milik ambaye ni majeruhi. Straika huyo rai wa Poland aliumia juzi wakati akiitumikia timu ya taifa na alikuwa akitarajiwa kufanyiwa vipimo jana ambapo inasemekana angekuwa nje ya uwanja kwa […]

Barcelona yafukuzia mabeki watano

MADRID, Hispania TIMU ya Barcelona inasemekana kuwa na mpango wa kufukuzia mabeki watano akiwamo wa kulia wa Arsenal, Hector Bellerin mwenye umri wa miaka 21. Mbali na beki huyo, gazeti la Marca liliripoti kuwa pia klabu hiyo inasemekana kuwafukuzia nyota wa Valencia, Joao Cancelo, 22, wa Bayern Munich, Joshua Kimmich, 21, wa Shakhtar Donetsk, Darijo Srna, 34 na anayekipiga katika […]

Schweinsteiger kutimkia Marekani Januari

LONDON, England STAA wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger, anasemekana kuwa na mpango wa kuitema klabu hiyo na kutimkia Marekani wakati wa usajili wa majira ya baridi yajayo. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, kwa sasa staa huyo mwenye umri wa miaka 32, anafanya mazoezi ya ziada ili kujiweka fiti kwa ajili ya kusaka timu baada ya kutemwa na kocha […]

Chelsea, Man City vitani kwa Aubameyang

LONDON, England TIMU za Chelsea na Manchester City  zinaripotiwa kwenye vita kali zikimwania staa wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye anawindwa pia  na Real Madrid. Kwa mujibu wa gazeti la Don Balon la nchini Hispania, klabu hizo mbili za Ligi Kuu England kwa sasa kila moja inahaha kumsajili raia huyo wa Gabon na kwamba kocha wa Man City, Pep Guardiola […]

Hazard kufanywa chambo kwa Bonucci

LONDON, England KLABU ya Chelsea inasemekana kuwa na mpango wa kumfanya chambo straika wake mahiri, Eden Hazard ili iweze kumnasa beki kisiki wa timu ya Juventus, Leonardo Bonucci wakati wa usajili wa majira ya baridi yajayo. Kwa mujibu wa taarifa za vyanzo vya habari kutoka ndani ya klabu hiyo, vilieleza jana kwamba beki huyo ambaye alisajiliwa na kocha Antonio Conte […]