LWANDAMINA AONYESHA VITU ADIMU YANGA

NA HUSSEIN OMAR KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, ameendelea kuonyesha vitu adimu kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana uliopo Posta jijini Dar es Salaam. Katika mazoezi hayo, Lwandamina alionyesha kuwa si mtu wa mchezo mchezo kutokana na kutoa vitu vya kipekee kwa nyota wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. […]

SIMBA YAKAMILISHA VIELELEZO VYA KESSY

NA ZAITUNI KIBWANA SIKU chache baada ya Simba kutakiwa vithibitisho vya kumlipa mishahara beki wake wa zamani, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na kusema wana kila karatasi iliyotakiwa kwenye sakata hilo. Simba iliombwa uthibitisho huo kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa, katika kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, kwamba Simba haina […]

SIMBA YAMALIZA TATIZO

NA ZAITUNI KIBWANA AMETUA mwanangu! Yule kipa mwenye rekodi ya kutwaa Taji la Dunia, ametua nchini jana tayari kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi, Simba kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Kipa huyo, Daniel Agyei (27), kutoka Ghana pia alikuwa kikwazo kikubwa kwa Yanga kupata ushindi kwenye mechi mbili za robo fainali ya Kombe la Shirikisho wakati akiwa langoni kuilinda Madeama. […]

CONTE AUKUBALI MUZIKI WA CHELSEA

LONDON, England KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte, anaonekana kuukubali muziki wa timu yake, baada ya kusema kuwa anavyoamini kwa sasa Chelsea ipo tofauti na si kama iliyofungwa na Arsenal na  Liverpool  Septemba, mwaka huu. Conte alitoa kauli hiyo juzi, baada ya kufikisha mechi ya saba bila kufungwa katika mchezo  waliopata  ushindi wa mabao 2-1   dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi. […]

GRIEZMANN AWAGWAYA MESSI, RONALDO TUZO YA  BALLON D´OR  

MADRID, Hispania STRAIKA wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, anaonekana kuwagwaya nyota wenzake, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, katika mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia,  Ballon d’Or, baada ya kusema kuwa ana nafasi ndogo kubeba  taji hilo kama vinara hao bado wapo kwenye gemu. Staa huyo wa  Barcelona na mwenzake wa  Real Madrid  wameshatwaa tuzo hiyo mara nane […]

ALEX SANCHEZ AZIDI KUMKUNA WENGER

LONDON, England   STRAIKA Alexis Sanchez anaonekna kuzidi kumkuna kocha wake, Arsene Wenger, baada ya Mfaransa huyo kusema kuwa amebaki ameduwaa kwa uwezo wake wa kubadili mchezo, baada ya kuiwezesha Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao  3-1 dhidi ya  Bournemouth, licha ya kuonekana kwa wengi kama amechoka. Kwa sasa  staa huyo raia wa Chile anaonekana kutakata tangu alipohamishiwa kwenye safu […]

MOURINHO AWEKA REKODI MBAYA KUPITA KIASI MAN UTD

  LONDON, England UNAWEZA kusema ni  majanga kutokana na matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu kwa timu ya Manchester United kuyapata tangu msimu wa  1990-91, baada ya kuambulia sare ya  bao  1-1  dhidi ya  West Ham United. Hali hiyo inatokana na kuwa klabu hiyo ya  Old Trafford  iliamua kumuajiri kocha wao, Jose Mourinho, msimu huu, baada ya miaka mitatu kukosa mafanikio […]