Yanga mtafanya kosa kubwa mkimtema Pluijm

  KATI ya mambo ambayo mara kadhaa yamekuwa yakiwachanganya wachezaji ni leo kuwa na kocha huyu na kesho wanashangaa kubadilishiwa mwingine na kubadilishiwa mifumo, hali inayowaacha njia panda. Kwa kawaida kila kocha ana mfumo na tabia zake, hivyo anapobadilishwa na kuletewa mwingine maana yake ni kwamba, wanaanza upya na bahati mbaya iwe huyo anayeletwa hajui mazingira ya ligi husika. Kama […]

Mayanga awashushia lawama washambuliaji

NA ZAINAB IDDY, BAADA ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salumu Mayanga, amewashushia zigo la lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kutumia nafasi walizopata. Akizungumza na BINGWA, Mayanga alisema hawakustahili kufungwa mabao hayo, kwani waliweza […]

Wachezaji Yanga wamkingia kifua Pluijm

NA ZAINAB IDDY, WAKATI kukiwa na  tetesi za Yanga kutaka kumbadilisha majukumu kocha wao mkuu, Hans van der Pluijm, kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo ya kusuasua Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, winga wa kikosi hicho, Simon Msuva, amesema tatizo si kocha bali ni uchovu wa wachezaji. Akizungumza na BINGWA juzi, Msuva alisema matokeo yanayopatikana yanatokana na wachezaji […]

Pluijm: Ilikuwa lazima Chirwa afunge bao

NA SALMA MPELI, KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema alimwandaa vya kutosha kisaikolojia mshambuliaji wa timu hiyo, Obrey Chirwa, ili aweze kufunga bao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Yanga ilishinda mabao 3-1 huku Chirwa akianza kufunga mengine yakiwekwa kimiani na […]

Ghafla Pluijm atajwa Azam

NA MWANDISHI WETU, SIKU chache baada ya BINGWA kufichua taarifa kuwa klabu ya Yanga inakaribia kumnasa kocha wa Zesco, Mzambia George Lwandamina, ghafla zimeibuka stori kuwa Azam wanasubiri miamba hiyo ya Jangwani ijichanganye kumtimua kocha huyo ili wao wampeleke Chamazi. Taarifa hizo zinadai kuwa jina la Pluijm liko kwenye akili za viongozi wa Azam ambao wameanza kuchanganywa na kufanya vibaya […]

Kamusoko afurahia unahodha Yanga

NA HUSSEIN OMAR, KIUNGO wa kimataifa wa Yanga Mzimbabwe, Thaban Kamusoko, amefurahishwa na kitendo cha kocha wake, Hans van der Pluijm, kumpa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kamusoko alivaa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huo ambao mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Yanga walionekana kurejesha makali yao […]

Kichuya ‘abatizwa’ jina la ‘Mwendo Kasi’

GEORGE KAYALA NA MWANI NYANGASA, MBEYA STRAIKA hatari wa Simba kwa sasa, Shiza Kichuya, amebatizwa jina la ‘Mwendo Kasi’ na mashabiki wa soka mkoani Mbeya kutokana na kasi yake aliyoionyesha kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu. Jina hilo alibatizwa rasmi juzi katika mechi kati ya timu yake na Mbeya City iliyofanyika katika Uwanja wa Sokoine […]