Kayala kuipeleka ‘Siwema’ Tabata Kisiwani

NA MWANDISHI WETU, MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini, George Kayala, Jumapili anatarajia kutumbuiza katika Kanisa la Africa Inland Church (AIC) lililopo  Tabata Kisiwani karibu na Uwanja wa Twiga jijini Dar es Salaam, akiwa na mtumishi wa Mungu, Paul Yunja. Kayala, ameliambia Papaso la Burudani kuwa siku hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwa mashabiki wake kununua DVD za albamu yake […]

Diamond ampa mil 2/- aliyetobolewa macho

NA MWANDISHI WETU, NYOTA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, jana amemkabidhi shilingi milioni 2 kijana Said Ally aliyeshambuliwa kisha kutobolewa macho yote mawili na mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, hali iliyopelekea kutoona tena. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena kinachoruka kupitia Clouds Fm wakati akimkabidhi fedha hizo, Diamond Platnumz  alimsihi Said kutojiona mpweke na akampa ahadi kuwa […]

Fanya hivi ili furaha itamalaki katika penzi lako

MIGOGORO ya mara kwa mara katika mapenzi wakati mwingine huwa inapelekea mapenzi baina ya wawili wapendanao kuchuja. Kuchuja huku kwa mapenzi si kwamba ni tukio ambalo huwa linafurahiwa sana na wahusika, hapana. Bali hujikuta tayari kuwa limetokea kutokana na nafsi zao zenyewe kuwa zimechoshwa na maudhi pamoja na kero za mara kwa mara katika mahusiano. Kwa bahati mbaya kwa wengi […]

Upendo kushinda Ufahamu [18]

Ilipoishia jana Uamuzi aliokuwa ameufikia ni kuamua kumfuata Roika nchini Mexico, akijua kuwa Roika yuko huko kikazi. SASA ENDELEA NCHINI HAITI UZIMA ndani ya kidonda cha mapenzi ulianza kuonekana kwa Roika. Alijiona mwepesi kidogo tofauti na siku zote. Kuwepo pembeni ya Ramona kulimpa matumaini makubwa ya kufanikiwa kumuoa mrembo huyo wa dunia. Siku hiyo walikuwa wametoka nje ya hoteli ya […]

Boateng anataka unahodha Bayern

MUNICH, Ujerumani BEKI Jerome Boateng amedai kuwa ndoto yake ya muda mrefu ni siku moja kuwa nahodha wa kikosi cha Bayern Munich. “Ningefurahia kuwa nahodha wa Bayern. Kama ingekuwa hivyo, kwangu, ingekuwa ni ndoto iliyotimia na heshima pia,” alisema Boateng, alipokuwa akihojiwa na gazeti la Bild. Wakati Bastian Sweinsteiger alipostaafu kucheza soka la kimataifa, nyota huyo mwenye umri wa miaka […]

Bosi Arsenal aingiza bil. 5/- kwa mwaka

LONDON, England MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis, ameshika nafasi ya pili kwenye orodha ya mabosi wanaolipwa mishahara minono pale England. Kwa mujibu wa takwimu, mwaka jana Gazidis aliweka mfukoni pauni milioni 2.648 (zaidi ya Sh Bil 5) na hiyo inamfanya kuwa bosi anayelipwa fedha nyingi nyuma ya Ed Woodward wa Manchester United. Hata hivyo, akaunti ya Gazidis […]

Mashabiki Liver, Man United wapigwa mkwara

MERSEYSIDE, England LIVERPOOL na Manchester United zimewataka mashabiki wao kuacha vitendo vya vurugu wakati timu hizo zitakapovaana keshokutwa. Man United na Liver watavaana katika mchezo wa Ligi Kuu England, utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Anfield. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kuelekea mchezo huo, shabiki atakayenaswa na kamera akifanya vurugu ataingia kwenye mikono ya polisi. “Kuna upinzani mkubwa kati ya timu […]

Emirates wafunika Ulaya kwa mapato

LONDON, England Arsenal imeongoza kwa klabu 10 zilizopata kipato kikubwa kutokana na viingilio vya uwanjani kwenye soka la Ulaya, kwa mujibu wa mtandao wa Deloitte. Mapato hayo yamejumuishwa kwenye msimu wa 2014/15 na uwanja wa klabu hiyo ya Arsenal, Emirates umeongoza. Takwimu hizo za mapato zilizokusanywa msimu mzima, zinaonyesha Uwanja wa Emirates umeingiza Euro milioni 132 (asilimia 30 ya faida […]

Serge Aurier amuokoa mchezaji aliyemeza ulimi

Bouake, Ivory Coast BEKI wa Ivory Coast, Serge Aurier, ameokoa maisha ya kiungo wa Mali, Moussa Doumbia, aliyekuwa amemeza ulimi. Mchezaji huyo wa klabu ya Paris Saint-Germain, Aurier, ambaye baadaye alishutumiwa kwa jinsi alivyoshangilia bao, alimuwahi Doumbia na kuuvuta ulimi na kumlaza vizuri baada ya kuangukia uso. Doumbia aliangukia uso baada ya kugongana na beki wa Sunderland, Lamine Kone. Kocha […]

Pogba awakimbiza Ozil, Sanchez

MANCHESTER, England KIUNGO Paul Pogba amewakimbiza wachezaji wenzake wa Ligi Kuu England kwa mauzo ya jezi. Manchester United walimnunua kiungo huyo kwa pauni milioni 89 majira ya kiangazi na kumnasa nyota huyo wa Ufaransa na sasa fedha yao waliyoitumia imerudi kutokana na mauzo ya jezi ya mchezaji huyo. Zlatan Ibrahimovic anashika nafasi ya pili, akifuatiwa na nyota wa Arsenal, Alexis […]