Mourinho ataja kilichoiponza Ajax kwa Spurs

AMSTERDAM, Uholanzi  KOCHA Jose Mourinho, amekitaja kilichoiponza Ajax na kusababisha itolewe katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Tottenham akisema ni kutokana na kung’ang’ania falsafa yao ya kucheza soka la kushambulia.  Katika mchezo huo wa marudiano  uliopigwa mjini Amsterdammers, Ajax walifanikiwa kuwa mbele kwa mabao  2-0 dhidi ya Tottenham, yaliyofungwa kipindi cha kwanza na nahodha wao,  Matthijs de Ligt […]

Katwila atolea macho nafasi ya nne TPL

NA MWANDISHI WETU KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema watahakikisha wanakuwa makini kwa mechi zilizosalia ili wamalize wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mtibwa Sugar juzi walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya JKT Tanzania, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro. Akizungumza na BINGWA jana, Katwila, alisema ligi inaenda ukingoni na ukiangalia […]

Okwi amvulia kofia Kagere

NA WINFRIDA MTOI PAMOJA na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kupiga ‘hat trick’ dhidi ya Coastal Union, lakini amejitoa kwenye mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kumwachia Meddie Kagere, ambaye naye pia alipiga ‘hat trick’ katika mechi hiyo. Okwi alisema mabao matatu aliyofunga dhidi ya Coastal Union yamechangiwa na ushirikiano mkubwa wa kikosi hicho katika kutengeneza  […]

Mamilioni yamwagika Yanga

NA WINFRIDA MTOI SIKU chache baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, hatimaye mamilioni yameanza kumwagika baada ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Yono Kevela, kutoa Sh milioni 20 kwa uongozi mpya ulioingia madarakani. Yono alikabidhi fedha hizo jana kwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela, kwenye ofisi za Yono Auction Mart, zilizopo […]

NDIYO ZAO Barca kitu gani, mbona Liverpool kupindua meza kawaida tu!

MERSEYSIDE, England UKWELI ni kwamba hakuna aliyekitarajia kilichotokea usiku wa kuamkia jana pale Anfield, wakati Liverpool wakifanikiwa kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza kule Hispania, wengi walisubiri kuiona safari ya Liver ikiishia Uingereza mbele ya wakali Barcelona. Badala yake, Liver wakiwa bila mastaa wake wawili, Roberto Firmino na Mohamed Salah, […]

GARI LIMEWAKA Samatta ameibeba tuzo iliyowatoa wakali kibao Ulaya

NA HASSAN DAUDI NYOTA ya nahodha wa Taifa Stars imezidi kung’ara huko barani Ulaya na hiyo ni baada ya juzi kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora kwa Wanasoka wenye asili ya Afrika, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji. Samatta mwenye umri wa miaka 26, aliinyakua tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwa kikosi cha Genk msimu huu, akiwa […]

Hellen Sogia kuweka wakfu kazi zake

NA BRIGHTER MASAKI MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini na mtumishi wa Mungu, Hellen Sogia, anatarajia kuweka wakfu kazi zake mbalimbali Julai 7, mwaka huu katika Ukumbi wa B. Mellin (Tumbi), Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na Papaso la Burudani, Helles Sogia alisema tukio hilo maalumu la kihistoria katika maisha yake ya utumishi kama ambavyo alivyoitwa na kuagizwa na Mungu, litasindikizwa […]